Wakulima wakumbukwa msimu huu wa mavuno, kukopeshwa magari

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya magari ya TATA Tanzania imezindua mpango  maalum  kwa ajili ya sekta ya usafirishaji  wa mizigo mikubwa  nchini kwa kuzindua Trela za mizigo aina ya ‘Tiva Trela’ ambalo unaweza kuzipata kwa mkopo ili kumrahisishia  mfanyabiashara na mkulima  katika kupakia mizigo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi  uliofanyika kwenye  ofisi za kampuni hiyo Vingunguti jijini Dar es Salaam,  Meneja Mauzo na  Masoko, Smart Deus amesema  lengo  la mpango huo ni kuwaweka karibu wateja na kampuni katika  msimu  huu wa mauzo  na mavuno nchini ambapo magari hayo yanapatikana kwa mkopo pia.

” Uzinduzi huu umeambatana  na uzinduzi wa Trela ya kubebea mizigo mikubwa kwa wakati mmoja. Pia tumeandaa mpango maalumu  kwa wateja watakaowahi kipindi hiki cha mwanzo kielekea msimu wa mauzo,” amesema.

Meneja mauzo na masoko wa kampuni ya TATA  ,Smart Deus (kulia) akibonyeza puto kuashiria Uzinduzi wa msimu mpya wa Biashara na Trela za mizigo  mikubwa aina ya TIVA  kuelekea msimu wa mavuno jijini Dar ees salaam jana.Wengine ni Robbert Mwakibibi Meneja magari mauzo wa magari makubwa na Begumisa Egbert (katikati)

Ameeleza kuwa kuanzia mwaka2021 hadi 2024 katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia  Suluhu Hassan, umekuwa ni wakati mzuri biashara kutokana na milango ya kibiashara kufunguka.

Deus amesema kutokana na hali hiyo wameahidi kushirikiana na Serikali na wadau wao kwa kuleta bidhaa bora zaidi zinazokidhi mahitaji ya watanzania.

Amesema kwa zaidi ya miaka 20 ya kampuni hiyo nchini, wamebaini uwepo wa changamoto katika usafirishaji kulingana na mazingira na barabara , hivyo kuja na suluhisho la kuleta magari yenye uwezo wa kuendana na mazingira hayo.

Naye  Meneja Mauzo wa TATA, Kitengo cha Force Motors, Robert Mwakabibi amesema mpango huo   haujaacha nyuma usafirishaji wa abiria baada ya kuleta gari salama kupunguza adha ya usafiri na kuwaongezea kipato wamiliki na madereva wa daladala.

Kwa upande wa magari ya shule amesema  wamebaini magari mengi hayakutengenezwa na mfumo mzuri kwa ajili ya wanafunzi hali iliyowapa msukumo wa kufanya mapinduzi katika sekta hiyo.

“Ukiangali gari zetu ni tofauti na nyingine, gari nyingi zinaletwa zikiwa zina muda mrefu lakini za kwetu ni gari mpya kabisa.  Gari za shule nyingi zilizopo hazijatengezwa maalum kwa ajili ya wanafunzi , sisi tumekuja na mfumo wa kuhudumia wanafunzi wa aina zote, wa kawaida na wenye mahitaji maaalum.

“Kwa kuzingatia changamoto ya usafiri wa abiria, kampuni imeleta  gari bora zinazoweza kupunguza adha ya usafiri pamoja na kuongeza kipato cha wamiliki wa daladala. “Tumeona soko linauhitaji mkubwa kwa usafiri wa wanafunzi, taasisi za serikali na binafsi,” ameeleza Mwakibibi.

Amesema wameweka mfumo mzuri wa  mteja kupata gari hizo ambapo kuna kulipa fedha taslimu na mkopo kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha.

Akizungumzia jinsi utaratibu  mkopo wa magari hayo unavyotolewa, Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Begumisa Egbert, amesema mkopo usio na riba unatakiwa kulipa   asilimia 50 na nyingine iliyobaki  inalipwa kwa kipindi cha miezi 12.

Ameeleza kuwa mkopo mwingine ambao utakuwa na riba kidogo, unatakiwa kulipa asilimia 20 ya bei ya gari unayotaka, kisha iliyobaki inalipwa kwa kuanzia miezi sita hadi  miaka mitatu.

spot_img

Latest articles

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

More like this

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...