Yanga haina imani na TFF, Bodi ya Ligi, yasisitiza haichezi Dabi

Na Mwandishi Wetu

Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema hauko yatari kupeleka shauri kwenye Kamati za Mamlaka za soka  ndani  kama iliyoelekezwa na Mahakama ya  Kimataifa ua Usuluhisi wa Michezo (CAS), ikihofia dhuluma, huku ikisisitiza kutocheza mechi ya’derby’.

CAS ilielekeza Yanga  kurudi kwenye Kamati za ndani kabla ya kurudi katika mahakama hiyo kwa ajili ya rufani.

Katika taarifa ambayo klabu hiyo imeitoa leo   Mei 5, 2025imesema  msimamo wao juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Bara uko pale pale wa kutoshiriki mechi hiyo kwa namna yoyote.

“Kutokana na uonevu na uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya  timu unaondelea kufanywa na Mamlaka za soka  Tanzania, Uongozi wa Yanga hauna imani na hauko tayari kupeleka shauri hilo kwenye Mamlaka ambao zinatenda dhulma,” imesema.

Kupitia Taarifa hiyo,uongozi wa Wanajangwani hao,umewataka Wanayanga kuwa tayari kuipambania haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhuluma na uvunjwaji wa kanuni unaondelea  kwa maslahi mapanda ya soka nchini.

Ikumbukwe kuwa Yanga ilifungua shauri la madai CAS  kwa kutoridhishwa na kitendo cha kuahirishwa kwa mchezo wake dhidi ya Simba uliokuwa uchezwe Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga iliwasilisha shauri la kuomba mechi hiyo isipangiwe tarehe nyingine hadi uamuzi utakapotolewa na Makahama hiyo. Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya  Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania na Klabu ya Simba.

Hata hivyo CAS iliijibu Yanga kwa kuitaka kurudi katika Kamati za Mamlaka za soka ambapo muda mfupi baadaye Bodi ya Ligi ilitangaza kutoa ratiba mpya ya  Ligi Kuu ikiwamo mchezo huo uliahirishwa wa Yanga na Simba.

spot_img

Latest articles

Jeuri ya ushindi CAFCL Simba waanza ‘kuchonga’

Na Winfrida Mtoi Ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika mchezo wa Ligi ya...

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this