Na Mwandishi Wetu
Jumla ya waogeleaji sita chipukizi wa Lake Victoria Sports Club ya jijini Mwanza wanatarajiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya kuogelea ya Kimataifa yatakayofanyika kesho Aprili 18 hadi 20, 2025 Dubai.
Waogelaji hao wameahidi kufanya vizuri katika mashindano hayo ili kuitangaza Tanzania Kimataifa.

Timu hiyo iliondoka nchini jana Aprili 16, 2025 ambapo tayari inaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mashindano nchini humo.
Waogeleaji hao walioondoka ni Ethan Makalla, Nusrat Hassan, Nasri Hassan ,. Ibrahim Igoro, Tahir Isak ,. Zeeshan Isak, Naseeb Hassan.