🔴🔴 Wananchi waguswa na miradi ya elimu inayotekelezwa na TAWA Liwale

📍Wakiri uhifadhi kuwa na manufaa

Na Mwandishi wetu, Lindi

MIRADI ya ujenzi wa madarasa mawili yenye thamani ya shillingi millioni 60 katika kijiji cha Ngumbu wilaya ya Liwale mkoani Lindi inayotekelezwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA chini ya ufadhili wa ushirika wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) na Tanzania umeibua matumaini mapya katika Sekta ya elimu Kwa jamii hiyo inayozunguka Hifadhi ya Selous.

Wakizungumza katika nyakati tofauti Aprili 14, 2025 wananchi hao wamesema ujenzi wa madarasa utapunguza uhaba wa miundombinu ya kielimu, kuongeza Ari ya kusoma na kuibua ndoto na matumaini mapya ya mafanikio ya kitaaluma kwa wanafunzi.

“Sasa tunakwenda dunia ya tatu, dunia inayomtaka mwanafunzi akae asome katika sehemu nzuri, apate taaluma nzuri ili aweze kujifunza vizuri. Kwahiyo Kitendo cha kupata haya madarasa ninawashukuru sana TAWA na wafadhili wanaoshirikiana nao” amesema Faraji Saidi Diwani wa Kata ya Kibutuka.

Kamanda wa TAWA Kituo cha Liwale, Philipo Urio amesema mradi huo umetokana na fedha za dharura za UVIKO 19 Kwa lengo la kusaidia shughuli za uhifadhi katika Pori la Akiba Selous na Hifadhi ya Taifa Nyerere na kwasasa umefikia asilimia 97 na unatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi huu wa Aprili tayari Kwa kuanza kutumika rasmi.

Amesema Kijiji cha Ngumbu kilichopo Kata ya Kibutuka kimezungukwa na Pori la Akiba Selous na hivyo kuwa wanufaika wa moja Kwa moja na fursa zitokanazo na uhifadhi zinazolenga kujenga uhusiano mzuri baina ya jamii na rasilimali za Taifa wakiwamo wanyamapori hususani tembo.

Mkuu wa wilaya ya Liwale, Goodluck Mlinga amepongeza jitihada za TAWA katika kuboresha huduma za kijamii Kwa wananchi hatua ambayo inasaidia kuongeza uhusiano mzuri baina ya wananchi na rasilimali za Taifa hususani wanyamapori.

“Hii itaisaidia nini?, Kwanza wananchi kuheshimu wanyamapori maana mwanzoni wananchi walikuwa hawaheshimu wanyama, wakiwaona wanajua ni maadui, lakini sasa hivi na wenyewe wanashiriki kwenye uhifadhi.

“Lakini Pili wananchi watashiriki katika utoaji wa taarifa za ujangili maana yake sasa wanaona wanyama ni Kinga Kwa ajili yao,” amesema Mlinga.

Naye Katibu wa Mbunge wa Liwale, Jaizu Abdallah ametambua mchango wa TAWA kwenye wilaya ya Liwale na kusema kuwa kitendo cha kujenga vyumba hivyo vya madarasa shule ya msingi Ngumbu ni hatua nzuri ya kuboresha mazingira ya watoto kupata elimu bora.

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii Kwa kutoa mazingira wezeshi Kwa wadau mbalimbali wa uhifadhi Kwa jili kutekeleza majukukumu yao hasa ya kiuhifadhi kama ilivyo Kwa Kijiji cha Ngumbu.

“Tuna kila sababu ya kushukuru wadau wetu lakini pia Serikali Kwa namna inavyoshirikiana na wadau hawa na leo tunaweza kuona matokeo makubwa ambayo yanatokana na hizi shughuli ambazo zinafanywa na wadau wetu katika maeneo yetu. Kijiji cha Ngumbu sasa kinashuhudia matokeo chanya ya jitihada za uhifadhi” alisema Maganja.

spot_img

Latest articles

Waogeleaji wa Lake Victoria Sports Club waahidi kuing’arisha Tanzania Kimataifa

Na Mwandishi Wetu Jumla ya waogeleaji sita  chipukizi wa Lake Victoria Sports Club  ya jijini...

Mbunge Kimei kinara kuzungumzia mahitaji ya wananchi

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei ametajwa kuwa...

Sekta binafsi zatakiwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mikakati mbalimbali ya nchi

Na Tatu Mohamed, Mwanza  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Stanislaus Nyongo...

Kafulila: Hatuwezi kujenga uchumi wa nchi bila kushirikisha sekta binafsi

Na Tatu Mohamed, Mwanza MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma...

More like this

Waogeleaji wa Lake Victoria Sports Club waahidi kuing’arisha Tanzania Kimataifa

Na Mwandishi Wetu Jumla ya waogeleaji sita  chipukizi wa Lake Victoria Sports Club  ya jijini...

Mbunge Kimei kinara kuzungumzia mahitaji ya wananchi

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt Charles Stephen Kimei ametajwa kuwa...

Sekta binafsi zatakiwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mikakati mbalimbali ya nchi

Na Tatu Mohamed, Mwanza  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Stanislaus Nyongo...