SIMBA YAIFUATA AL MASRY NA HESABU KALI

Na Winfrida Mtoi

Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka Machi 28,2025 kuifuata timu ya Al Masry nchini Misri kwa mchezo wao wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika huku uongozi wa klabu hiyo ukiwa na hesabu za kutinga nusu fainali.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Habari na Mawasiliano wa hiyo, Ahmed Ally amesema malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanavuka hatua ya robo fainali na kutinga nusu fainali.

Ahmed amesema licha ya kukutana na mpinzani mgumu hatua ya robo fainali lakini wamejipanga kuhakikisha wanavuka na ndiyo sababu ya kuja na kauli mbiu ya ‘Hii tunavuka’.

“Kwa miaka mitano mfululizo tumekuwa tukiishia robo fainali kwenye michuano ya Afrika lakini safari hii tumedhamiria kuhakikisha tunavuka,”amesema Ahmed.

Aidha amesema wachezaji waliokuwa sehemu ya timu ya taifa, Taifa Stars, wataungana na wenzao nchini Misri ili kukamilisha maandalizi ya mchezo huo wakati Camara na Mukwala, tayari wamewasili na kuungana na wenzao kwa maandalizi zaidi kabla ya safari.

spot_img

Latest articles

WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSIMAMIA UCHAGUZI KWA UFANISI

Na Mwandishi Wetu, Tabora TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa watendaji wa...

DAWASA YATEGUA KITENDAWILI GHARAMA UONDOSHAJI MAJITAKA KIGAMBONI

Na Mwandishi Wetu WAKAZI wa Kigamboni wanatarajiwa kupunguza gharama za uondoshaji wa majitaka baada...

TANZANIA NA OMAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA WANAHABARI KUPITIA KONGAMANO LA OKTOBA MOSI

DAR ES SALAAM Chama cha Waandishi wa Habari cha Oman (OJA), kwa kushirikiana na Chama...

C-CEOs Forum kuwa chachu ya utekelezaji wa Dira 2050

Na Mwandishi wa OTR Arusha. Serikali imesema Mkutano wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu...

More like this