Tanzania na Misri kuendeleza ushirikiano kwenye miradi ya umeme

📌Waziri wa Mambo Nje Misri atembelea Bwawa la Julius Nyerere

📌Asifu hatua za Rais wa Tanzania na Misri kusimamia utekelezaji wa mradi

📌Mradi wafikia asilimia 99.89

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano kwenye utekelezaji wa miradi ya umeme na kudunisha ushirikiano uliowekwa na waasisi wa nchi hizo.

Kapinga ameyasema hayo leo Machi 20, 2025, mkoani Pwani wakati alipofanya ziara katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri waishio nje ya Jamhuri ya Misri, Dkt Badir Abdelatty ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Waziri Badir na ujumbe wake.

“Tunamshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa msingi imara wa utekelezaji wa miradi huu wa umeme na tumeona matunda halisi ya usimamizi wake,” amesema Kapinga.

Amesema nchi ya Misri imetekeleza mradi huo wa JNHPP kwa kuzingatia matakwa ya nchi ya Tanzania ambapo mpaka sasa mashine nane kati ya tisa zimewashwa na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa JNHPP, Waziri, Dkt. Badir Abdelatty, amesifu ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Misri na kuishukuru Tanzania kwa kuiamini nchi yake kutekeleza mradi huo wa JNHPP, kwani utawanufaisha wananchi wa Tanzania walio wengi hususani wale wanaozungukwa na eneo la mradi.

Amesema nchi za Afrika zinapaswa kujivunia uwepo wa miradi ya umeme kwa maendeleo ya waafrika wenyewe na kuahidi kuwa Misri itaendeleza ushirikiano na Tanzania kwenye utekelezaji wa miradi mingine kama hiyo Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Dannis Londo amesema, Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ulionao ili kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi hususani kwenye miradi ya sekta ya Nishati.

Ziara hiyo imehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi wa Misri nchini Tanzania, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mafuta, Dkt. James Mataragio, na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

spot_img

Latest articles

Mapato yasiyo ya kodi yafikia asilimia 67, OMH yadhamiria kufikia lengo la mwaka

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), imeendelea kuonesha mafanikio...

Dkt. Biteko: Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kufikia asilimia 75 mwaka 2030

Na Mwandishi Wetu 📌 Dkt. Biteko akutana na Balozi wa Japan nchini 📌 Tanzania na...

Twange aanza kazi rasmi Tanesco

📌Aomba ushirikiano ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na umeme wa uhakika. 📌Aahidi Kuendeleza Mazuri yaliyofanyika...

Shirika la Posta Tanzania lashiriki kongamano la eLearning Afrika, laja na huduma ya Swifpack

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Posta Tanzania ni miongoni mwa washiriki katika kongamano la...

More like this

Mapato yasiyo ya kodi yafikia asilimia 67, OMH yadhamiria kufikia lengo la mwaka

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), imeendelea kuonesha mafanikio...

Dkt. Biteko: Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kufikia asilimia 75 mwaka 2030

Na Mwandishi Wetu 📌 Dkt. Biteko akutana na Balozi wa Japan nchini 📌 Tanzania na...

Twange aanza kazi rasmi Tanesco

📌Aomba ushirikiano ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na umeme wa uhakika. 📌Aahidi Kuendeleza Mazuri yaliyofanyika...