Lina PG Tour msimu wa pili yaanza kulindima leo, wachezaji 122 wajitokeza kushiriki

Na Mwandishi wetu

WACHEZAJI takribani 122 wamejiandikisha kushiriki mashindano ya Lina PG Tour msimu wa pili yanayoanza kutimua vumbi leo katika Viwanja vya gofu vya Gymkhana mkoani Morogoro.

Mashindano hayo ambayo kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka jana yanaendelea tena mwaka huu yakiwa na lengo la kumuenzi mchezaji gofu wa zamani timu ya Taifa ya wanawake marehemu Lina Nkya ambaye alikuwa na mapenzi makubwa na mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kiongozi wa mashindano hayo, Ayne Magombe amesema kati ya wachezaji hao waliojiandikisha kushiriki 47 ni wachezaji wa gofu wa kulipwa na chipukizi huku 75 wakiwa wachezaji wasindikizaji.

Amesema mashindano hayo yameanza leo na yanatarajiwa kumalizika Machi 2, 2025 na kwamba yanafanyika kila mwaka kwa kujumuisha klabu za wachezajii wote wanaopenda kushiriki mchezo huo kutoka maeneo mbalimbali nchini.

“Mashindano haya yameandaliwa na familia ya Said Nkya katika kumuenzi mama Lina, yatafanyika kwa siku nne yakihusisha mashimo 72, hivyo niwaombe wapenzi wote wa mchezo wa gofu hasa waliopo Morogoro na sehemu mbalimbali kujitokeza kushiriki. Kwa pamoja tuongeze ujuzi zaidi, kukuza vipaji na vipato vya wachezaji wetu,” amesema na kuongeza:

“Mashindano ya Lina Tour yatakuwa ni endelevu, kwa sasa tuna mashindano matano kwa mwaka, lakini tukipata sapoti kwa wadau wengine tunaweza kuwa na mashindano mengi zaidi ili kukuza huu mchezo,”.

Naye mchezaji wa gofu wa kulipwa kutoka klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Fadhil Nkya amesema kila mtu ana uwezo wa kucheza mchezo huo hivyo ameitaka jamii kuondoa dhana kuwa mchezo huo uchezwa na matajiri.

“Kila mtu anauwezo wa kucheza mchezo huu na uwepo wa mashindano kama haya ya Lina inatusaidia wachezaji kufanya mazoezi ya kutosha ambayo yanatusaidia kufanya vizuri wakati wa kushiriki mashindano makubwa nje ya nchi,” amesema Nkya.

Amesema kwa siku mchezaji wa gofu ulenga mashimo 18, kwa siku nne watakazocheza katika mashindano watalenga jumla ya mashimo 72 na ili mtu awe mshindi lazima amalize mashino yote na afanye vizuri kuliko wengine.

“Kwa miaka mitano ijayo naiona gofu kuja kuwa kubwa sana na wadau wakijitokeza kutusaidia tunaweza kufanya makubwa, tumeanza mwaka jana lakini matokeo mazuri yamejitokeza, tunawaomba watu wajitokeze kushiriki huu mchezo,” amesema Nkya.

Kwa upande wake Mchezaji wa kulipwa wa gofu kutoka klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Hassan Kadio amesema amejiandaa vizuri na upande wa wachezaji wa kulipwa kupitia michuano hiyo wamepata bahati ya kujiweka vizuri katika kushiriki mashindano ya kimataifa.

“Mashindano haya yametufanya tunakuwa bize sana na tumeamua kuweka nguvu zetu kwa ajili ya kushiriki Lina PG Tour, tunaomba wachezaji wengine kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki pia,” amesema Kadio.

spot_img

Latest articles

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...

Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ya Sabasaba kutangaza huduma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ...

More like this

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...