Tanzania, UNODC kushirikiana kukabili uhalifu unaoathiri Mazingira

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Ofisi ya Kanda ya Afrika Mashariki (UNODC ROEA), imejipanga kushirikiana zaidi katika kupambana na uhalifu unaoathiri mazingira yanayolinda bayoanuwai.

Hayo yamebainishwa leo Februari 17, 2025 katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dkt. Pindi Chana na Mwakilishi wa Kanda wa UNODC ROEA, Ashita Mittal.

Akizungumza katika kikao hicho Chana amesema kupitia kikao hicho Wizara ya Maliasili na Utalii na UNODC wamepata fursa ya kuangalia jinsi UNODC inavyounga mkono juhudi za Tanzania za kukabiliana na uhalifu unaoathiri mazingira, kuangazia miradi inayoendelea, ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa wanyamapori, uhalifu wa uvuvi na juhudi za usalama wa baharini.

Pia, Chana ametumia fursa hiyo kutoa shukrani zangu za dhati kwa UNODC kwa msaada wa kifedha na kiufundi unaotolewa kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kupambana na uhalifu wa kimataifa.

“Biashara Haramu ya wanyamapori sio tu inaleta vitisho vya usalama kwa urithi wetu wa asili lakini pia inadhoofisha juhudi za uhifadhi wa bioanuwai miongoni mwa nchi wanachama ambapo umeathiri vibaya uchumi wetu na kuzidisha uhalifu mwingine wa kupangwa kama vile utakatishaji fedha, ufisadi, dawa za kulevya na biashara haramu ya silaha kutaja machache”, ameeleza.

Kwa upande wake, Ashita Mittal ameahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa mafunzo ya kujengea uwezo kuhusu namna ya kukabiliana na biashara haramu ya wanyamapori huku akisisitiza kuwa ni muhimu kushirikiana kwa pamoja kutatua changamoto hiyo.

“Hatuhitaji pesa nyingi lakini tunahitaji kuangalia namna ya kuwajengea uwezo watu wetu na kushirikiana na jamii katika kukabiliana na biashara haramu ya wanyamapori lakini tunahitaji wafadhili wa kutusaidia”, amesema Mittal.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

spot_img

Latest articles

Papa mpya apatikana ni Robert Prevost

Na Mwandishi Wetu Papa Mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, ametangazwa ni Kardinali Robert Francis Prevost(69),...

Waziri Masauni, Umoja wa Ulaya wajadili Mazingira

Mwandishi Maalum-Denmark Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad...

Serikali yasamehe faini za maji, yataka wananchi warejeshewe huduma

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametangaza msamaha wa faini zote kwa wananchi...

Spika wa Bunge ateta na Dk. Mwapinga, amhakikishia ushirikiano

Na Mwandishi Wetu Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani...

More like this

Papa mpya apatikana ni Robert Prevost

Na Mwandishi Wetu Papa Mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, ametangazwa ni Kardinali Robert Francis Prevost(69),...

Waziri Masauni, Umoja wa Ulaya wajadili Mazingira

Mwandishi Maalum-Denmark Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad...

Serikali yasamehe faini za maji, yataka wananchi warejeshewe huduma

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametangaza msamaha wa faini zote kwa wananchi...