Mahakama ya kijeshi DRC yatoa hati ya kukamatwa kiongozi wa M23

MAHAKAMA ya Kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa umoja wa makundi ya waasi nchini humo ya Alliance Fleuve Congo (AFC/M23), Corneille Nangaa.

Shirika la Habari la AP limeripoti leo Februari 7, 2025, kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo imetoa hati Nangaa akamatwe akituhumiwa kuhusika katika kile ilichotaja kuwa ni uasi na uhalifu wa kivita dhidi ya raia nchini humo.

Televisheni ya Taifa ya DRC nayo iliripoti kuwa hati ya kukamatwa kwa Nangaa imetolewa Jumanne Februari 4, 2025, baada ya kuhusika katika mauaji ya maelfu ya raia katika mapigano yaliyoibuliwa na wapiganaji wake katika Jimbo la Kivu Kaskazini nchini humo.

Mahakama hiyo katika hati yake imesema kutekeleza mauaji ya raia katika mapigano hayo ni kinyume cha sheria za nchi na sheria za kimataifa.Imeamuru Nangaa akamatwe akiwa mahali popote atakapokutwa duniani na kufikishwa katika Mahakama ya kijeshi nchini DRC.

spot_img

Latest articles

WINTZ YAWAFUNGULIA FURSA WANAWAKE WA KCMC KATIKA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA

Na Mwandishi Wetu JUMUIYA ya Wanawake katika Nyuklia Tanzania (WiNTz) imetembelea Hospitali ya KCMC...

CRDB Marathon yaendelea kuchochea afya, uwezeshaji vijana

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amesema Tanzania...

More like this

WINTZ YAWAFUNGULIA FURSA WANAWAKE WA KCMC KATIKA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA

Na Mwandishi Wetu JUMUIYA ya Wanawake katika Nyuklia Tanzania (WiNTz) imetembelea Hospitali ya KCMC...