Rais Mwinyi: SMZ kushirikiana na Madhehebu ya dini kuhubiri amani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameleeza kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na Madhehebu ya Imani zote kuhubiri Amani, kudumisha Upendo na Umoja ndani ya jamii kwani ndio Msingi wa mambo yote ya Maendeleo katika kila nyanja.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Februari 03, 2025 alipozungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Askofu Alex Malasusa na ujumbe aliofuatana nao waliofika Ikulu Zanzibar.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa Taasisi za dini zimekuwa na mchango mkubwa wa maendeleo ya jamii hivyo ni vema kwa Vvongozi na waumini kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani ili Serikali ifanye jukumu la kuleta maendeleo kwa Ufanisi.

Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kufarijika na mchango unaotolewa na KKKT ya jamii hususan katika masuala ya Afya, Elimu, Maji na Malezi ya yatima na kuwasisitiza kuendelea na michango hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa jamii.

Hata hivyo, Rais Mwinyi amelishauri Kanisa hilo kuwekeza katika sekta ya utalii, elimu, biashara na uwekezaji na Serikali iko tayari kushirikiana nao na kutoa kila msaada kufanikisha azma hiyo.

Vilevile Rais Mwinyi amepongeza juhudi za Kanisa kuwaendeleza vijana kielimu kupitia Chuo Kikuu cha Tumaini kwa Mafunzo mbalimbali na kuchangia kuzalisha Wataalamu Wazalendo pamoja na kuwa na wazo la kuanzisha Tawi la Chuo hicho Zanzibar.

Naye Askofu Alex Malasusa ambae pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ameshukuru Ushirikiano Uliopo baina ya Serikali na Kanisa hilo aliouelezea kuwa ni kichocheo cha mambo yote ya Maendeleo yanayaofanywa na Kanisa pamoja na kupongeza hatua za Maendeleo katika Ujenzi wa Miundombinu, Ubunifu na utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa Buluu kwa mafanikio na kudumisha amani na utulivu nchini.

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this