TANZANIA NA SOMALIA KUBADILISHANA WAFUNGWA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SERIKALI ya Tanzania na Somalia zimesaini mikataba miwili ya makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya ulinzi na usalama na kubadilishana wafungwa.

Mikataba hiyo imesainiwa leo Januari 29, 2025 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa kwa upande wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Ahmed Moalim Fiqi kwa upande wa Somalia.

Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo, Bashungwa amesema mkataba wa kubadilishana wafungwa utaziwezesha nchi hizo mbili kuruhusu wafungwa waweze kutumikia adhabu katika nchi zao na kusaidia kupunguza gharama za kifedha za kuwahudumia wafungwa hao.

“Inapotokea kuna Watanzania wenzetu wameingia katika hali ya kuwa wafungwa wakiwa kule Somalia, kupitia mkataba tuliosaini utatuwezesha kuwachukuwa Watanzania kuwaleta kwenye magereza yetu, vile vile kwa wafungwa wa Somalia watarudishwa kuendelea na vifungo vyao nchini kwao,” ameeleza.

Aidha, Bashungwa amesema mkataba wa ushirikiano kuhusu ulinzi na usalama, unalenga kuimarisha uwezo vyombo vya usalama kwa kutoa mafunzo kwa Askari wa pande zote mbili, kutekeleza operesheni za pamoja, kubadilishana utaalam katika masuala ya usalama na ulinzi pamoja na kubadilishana taarifa za kiintelijensia.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa amesema utiaji saini wa mikataba hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Somali, Hassan Sheikh Mohamud ili kuendelea kuimarisha ushirikiano.

spot_img

Latest articles

Aliyekuwa akiombewa amuua mchungaji wake kwa panga

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia Victor Fransis Thomas (39), mkulima...

Lissu awaambia wafuasi wake wajiandae akitoka ni mchakamchaka

Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa Chama Cha  Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amewaambia wasuasi na...

Wafanyakazi wa Majumbani 700 Watunukiwa Vyeti vya Mafunzo ya VETA

Na Tatu Mohamed ZAIDI ya wafanyakazi wa majumbani 700 wamepatiwa mafunzo maalum na kutunukiwa vyeti...

Kada wa CCM, Lameck Nyambara Ajitosa Ubunge Segerea

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lameck Nyambara amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo...

More like this