Dabi ya Kariakoo Wanawake, kitaumana kesho

Na Winfrida Mtoi

Mechi ya Dabi ya Kariakoo ya Ligi ya Wanawake Tanzania Bara, Yanga Princess dhidi ya Simba Queens inatarajiwa kupigwa kesho saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Simba Queens inaongoza ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda michezo yake yote mitatu ilicheza hadi sasa  wakati Yanga Princess ipo nafasi ya tano na alama tatu, ikiwa bado haijaonja ushindi tangu ligi imeanza ikitoka sare mechi zote tatu ilizocheza.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake mashabiki wa timu hizo kutokana na tambo zao hasa baada ya  klabu hizo mbili kwa sasa kuamua  kutumia uwanja huo kwa mechi zake nyumbani kwa timu zote za  wanawake na wanaume.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Yanga Princess ambayo ni mwenyeji wa mchezo, Edna Lema amesema wanaiheshimu Simba kutokana na ubora wake ikiwa inaongoza ligi hiyo na haijafungwa mchezo wowote.

“Sisi hatujapata matokeo mazuri ya mechi zetu za mwanzo lakini mechi ya Dabi ina mipango yake ya kuhakikisha unapata matokeo mazuri, sisi kama timu tupo tayari kwa mechi ya kesho,”  amesema Edna.

Kwa upande wake Kocha wa Simba Queens,Yussif Basigi amesema itakuwa ni mechi ya kuvutia na mipango yao ni kuonyesha mchezo mzuri na kupata matokeo ya ushindi.

“Wachezaji wote wako fiti na tayari kwa mchezo huo.Utakuwa ni mchezo mzuri na mgumu,tunahitaji kuwa makini kwenye maeneo yote ili kupata ushindi na kujiweka mazingira mazuri ya kuendelea kuongoza ligi,” amesema  Basigi.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika uwanja huo Oktoba 02,2024 katika mchezo wa nusu fainali wa Ngao ya Jamii ambapo Yanga ilishinda kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

spot_img

Latest articles

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yaweka wazi nafasi yake kwenye Uchaguzi Mkuu

Na Tatu Mohamed TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesema kuwa ina...

TMDA yaendelea kuelimisha umma juu ya matumizi sahihi ya dawa Sabasaba

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Imeendelea kutoa Elimu kwa...

Mazingira wezeshi ya Serikali yafungua fursa mpya za Uwekezaji kupitia TAWA

📍 Milango ya uwekezaji bado iko wazi Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usimamizi wa...

CRDB yamkabidhi Rahabu Mwambene zawadi ya gari aina ya Ford Ranger XLT 

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imemkabidhi Rahabu Mwambene zawadi ya gari aina ya Ford...

More like this