IAEA yaipongeza Zanzibar kwa Ushirikiano Katika Kilimo na Mifugo

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Suleiman Masoud Makame, ameshukuru Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) kwa namna shirika hilo linavyoisaidia Zanzibar katika sekta ya kilimo na mifugo.

Akizungumza katika ofisi za Wizara ya Kilimo Zanzibar baada ya kupokea ugeni kutoka IAEA, ugeni ulioongozwa na Bwana Gashaw Gebeyehu Wolde, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kiufundi kwa Afrika, pamoja na Bi. Azza Kashlan, Afisa wa Usimamizi wa Programu, Waziri Makame alisema wizara yake itaendelea kushirikiana kwa karibu na IAEA ili kuhakikisha ushirikiano huo unaimarika zaidi, kama ambavyo umefanikiwa katika maeneo ya mazao na mifugo.

Kwa upande wake, Bwana Gashaw Gebeyehu Wolde alisema kuwa IAEA ina miradi ya kitaifa nchini Tanzania katika sekta ya kilimo, na nia yao ni kuona miradi hiyo inaleta matokeo chanya kwa wananchi.

Naye Prof. Najat Kassim Mohammed, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), alieleza kuwa kulikuwa na mradi wa kilimo uliomalizika mwaka jana, na kikao kilichofanyika Zanzibar kitasaidia kufanikisha tafiti mpya zitakazosaidia kupambana na wadudu wanaoshambulia matunda, jambo litakalowaletea wananchi maendeleo ya moja kwa moja.

Ziara hiyo ilionyesha dhamira ya IAEA ya kuendeleza ushirikiano wake na Zanzibar, hususan katika sekta za kilimo na mifugo, ili kuongeza usalama wa chakula, kuboresha maisha ya wananchi, na kuimarisha maendeleo endelevu visiwani.

spot_img

Latest articles

JAB yazindua mwongozo wa kisheria wa utoaji wa Ithibati ya maisha kwa waandishi

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imezindua rasmi Mwongozo wa...

BRELA YAIBUA FURSA MPYA ULINZI WA ALAMA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Na Mwandishi Wetu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wajasiriamali wanaoshiriki...

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Dkt. Jafar Seif: Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sabasaba larahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za...

More like this