Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi yaanza kazi, yakaribisha wananchi kutoa maoni

Na Winfrida Mtoi

Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi nchini, imesema tayari imeanza kazi rasmi, hivyo kutoa wito kwa wananchi kutoa maoni ya kile wanachohotaji kifanyiwe maboresho katika mfumo wa ulipaji na ukusanyaji kodi.

Akizungumza leo Oktoba, 22 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa tume hiyo, Balozi Ombeni Sefue amesema wapo tayari kushirikiana na kumsikiliza kila mdau  iwe mmoja mmoja, kupitia vyama vya kitaalamu, jumuiya za biashara na nyingine ili kupata maoni yatakayowasilishwa kwa Rais Dk. Samia Suluhu.

Balozi Sefue amesema lengo ni kuhakikisha kunakuwa na mfumo bora wa kukusanya mapato na itafanya tathimini hiyo kwa kushirikisha wananchi.

“Mtakumbuka kuwa tarehe 4 Oktoba 2024, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizindua rasmi Tume ya Kutathmini na Kushauri kuhusu Maboresho ya Kodi.

“Kama mjuavyo Tume hii imeundwa kufuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji kuhusu kero mbalimbali zinazotokana na mfumo wa kodi nchini,” ameeleza  Mwenyekiti huyo.

Amefafanua kuwa Tume hiyo imepewa miezi sita lakini machakato wa kutoa maoni utachukua kipindi kisichopungua miezi miwili kuanzia sasa, baada ya hapo watachukua mapendekezo hayo, kuyafanyia tathmini na kuyachanganua kabla ya kuwasilisha kwa Rais.

Ameeleza kuwa wameandaa namna bora ya kuratibu  ushiriki wa wananchi, wafanyabiashara, wawekezaji na taasisi za umma na binafsi, asasi za kiraia, wadau wa maendeleo na wananchi wanaishi nje ya nchi ikiwamo kufanya mikutano katika maeneo mbalimbali.

Balozi Sefue amesema lengo la Serikali imedhamiria  kufikia kiwango  cha asilimia 15 ya pato la Taifa  ifikapo mwaka 2026/27  hatua itakayoongeza  uwezo wa nchi kugharamia miradi ya maendeleo na kupunguza kiwango cha utegemezi wa mikopo na misaada.



spot_img

Latest articles

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

Viongozi wa dini waendelea kihimiza amani uchaguzi mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam VIONGOZI wa dini nchini wameendelea kuhimiza umuhimu wa kudumisha...

More like this

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...