DCEA yakamata kilo 1,815 za skanka

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata watu watano kwa tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya kilogramu 1,815 aina ya skanka ambayo ni aina bangi ya kusindika yenye kiwango kikubwa cha kemikali yenye sumu aina ya Tetrahydrocannabinol (THC).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10, 2024 Jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali (DCEA),Aretas Lyimo, amesema watu hao wamekamatwa katika operesheni iliyofanyika Agosti 28, 2024 hadi Septemba 2, 2024 katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Amewataja watuhumiwa walikamatwa kuwa ni Richard Henry   Mwanri (47) ambaye ni Mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi Makonde Wilaya ya Kinondoni, Felista Henry Mwanri (70) mkulima na mkazi wa Luguluni Mbezi Wilaya ya Ubungo ambaye ni mmiliki wa nyumba zilipokutwa dawa za kulevya.

Watuhumiwa wengine ni Athumani Koja Mohamed (58) mfanyabiashara na mkazi wa Mkoa wa Tanga, Omary Chande Mohamed (32) dereva wa bajaji mkazi wa Buza pamoja na Juma Abdallah Chapa (36) mkazi wa Kiwalani.

Kamishna Jenerali Lyimo amesema kuwa katika operesheni hiyo pia wamekamata  gari aina ya Mitsubishi Pajero yenye namba za Usajili T551 CAB pamoja na bajaji yenye namba za usajil MC 844 CZV.

“Mtuhumiwa Richard Mwanri amekuwa akipokea dawa za kulevya za kutoka nchi mbalimbali na kuziingiza nchini kwa usafiri wa magari zikiwa zimefichwa kwa kuchanganywa na bidhaa nyingine kasha kusambaza kwa wauzaji” amesema.

Amefafanua kuwa dawa ya kulevya aina ya skanka ni aina bangi ya kusindika yenye kiwango kikubwa cha kemikali yenye sumu aina ya Tetrahydrocannabinol (THC) ambayo inaweza kuharibu mfumo wa fahamu, akili na kusababisha magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo moyo, figo na ini. Matumizi ya skanka kwa wajawazito inaweza kusababisha madhara kwa mtoto aliye tumboni ikiwemo kuathiri maendeleo ya ubongo na kuzaliwa na uzito mdogo.

spot_img

Latest articles

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

Waangalizi wa Uchaguzi watakiwa kutoingilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAANGALIZI wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa wametakiwa kuzingatia sheria...

More like this

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...