Milioni 300 zawekezwa kiwanda cha YLM Food Company Limited

Na Grace Mwakalinga

SHILINGI milioni 300 zimetumika kuwekeza kiwanda cha YLM Food Company Limited kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzalisha karanga za YY ambazo tayari zimeingizwa sokoni.

Kwa mujibu wa Meneja wa kiwanda hicho, Christopher Godfrey, amesema hadi sasa wamezalisha ajira zaidi 20 na kwamba wanaendelea kufungua fursa za ajira kupitia bidhaa hizo za karanga ambazo tayari zimewekwa sokoni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho , Mi Yuiing amemtangaza, muigizaji maarufu nchini, Shamsha Ford kuwa balozi wa bidhaa za Karanga za YY na kwamba wana imani na msanii huyo kutangaza bidhaa hizo nchini.

Aidha Yuiing ameeleza kufahishwa na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini ambayo yamemvutia kuwekeza sambamba na ziara za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan nchini China kuitangaza Tanzania katika fursa za kibiashara.

“Uwekezaji huu sio tu kwa ajili ya uzalishaji wa karanga, bali pia unatoa nafasi za ajira kwa vijana zaidi na tunatarajia kutoa fursa zaidi kwa watu hususani wanaohitaji uwakala wa bidhaa za karanga za YY,” alisema Yuiing.

Balozi wa YY Karanga, Shamsa Ford, amewataka wafanyabiashara na mawakala kuchangamkia fursa ya bidhaa hizo ili kujiingizia kipato na amewahakikishia wananchi kuhusu ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho.

“Kiwanda hiki kinatoa fursa kwa watanzania kujiajiri, kupata ajira, na kukuza uchumi kwa wale wanaotafuta fursa za biashara, uwekezaji huu ni hatua nzuri ya kuweza kuuza na kusambaza karanga,” amesema Shamsha.

spot_img

Latest articles

Safari ya ‘TLP’ ya Lissu ni ipi?

MWAKA 1992 wakati nchi hii ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kulikuwa...

Karibu 2025, tuyakatae magenge haya sasa

LEO ni siku ya pili katika mwaka mpya wa 2025. Ninawatakia wasomaji wa safu...

Kuubeba uozo wa 2024  kuingia 2025 ni fedheha

NI siku nne tu zimebakia kuupa kisogo mwaka 2024. Mwaka huu ulikuwa na mambo...

Hivi vikosi kazi vimerejea kwa mlango wa nyuma?

KUNA kila dalili kwamba taifa letu kidogokidogo linakumbwa na hali ya kutokuaminiana. Hali hii...

More like this

Safari ya ‘TLP’ ya Lissu ni ipi?

MWAKA 1992 wakati nchi hii ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kulikuwa...

Karibu 2025, tuyakatae magenge haya sasa

LEO ni siku ya pili katika mwaka mpya wa 2025. Ninawatakia wasomaji wa safu...

Kuubeba uozo wa 2024  kuingia 2025 ni fedheha

NI siku nne tu zimebakia kuupa kisogo mwaka 2024. Mwaka huu ulikuwa na mambo...