Mabasi 100 ya DART yaja, kadi kurejea mwezi ujao

Na mwandishi Wetu
SERIKALI inatarajia kuingiza mabasi mpya 100 nchini kwa ajili ya kuboresha hali ya usafiri wa mwendokasi jijini Dar es Salaam.

Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu amesema jijini Dar es Salaam leo Julai 15,2024 kwamba mpango huo utafanikishwa na benki ya NMB ambayo imekubali kuikopesha DART ili kuimarisha huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam.

Amesema mazungumzo ya kutiliana saini mkataba kwa kazi hiyo yatafanyika Dar es Salaam, Julai 16, 2024.

Mabasi hayo yanatarajiwa yawe yamefika nchini miezi sita ijayo na yatakuwa kwenye barabara kuu kwanza, kabla ya kuingia kwenye matawi.

Amesema, pamoja na mpango wa kuongeza mabasi, malengo ya kuimarisha huduma ya usafiri huo ni kuwa na watoa huduma zaidi ya mmoja, akifafanua kwamba huenda wakawa kati ya watatu hadi wanne, ambao watakuwa wanashindana kwa kuchukua barabara tofauti.

Amethibitisha kuwa kwa sasa DART inamilikiwa na serikali kwa aslimia 85, na kuelekeza kwamba huduma hiyo ilianza na mguu mbaya kwani pamoja na kuwa na ukiritimba wa barabara na abiria wa kutosha, ni ajabu kwamba ubora wa huduma siyo wa kuridhisha.

Mchechu amesema: “Kuna wizi wa mapato” amesisitiza kwamba mabadiliko makubwa sasa yanafanyika kwa kubadili mfumo wa kukata tiketi kutoka wa kutumia fedha taslimu kwenda usiotumia fedha hizo ili kupunguza wizi.

Amesema mfumo wa kutokutumia fedha taslimu utaanza kazi Agosti mwaka huu.

DART imekuwa katika changamoto kubwa jijini Dar es Salaam kwa muda sasa, kutokana na huduma mbovu kwa abiria inayochangiwa na uhaba wa mabasi na ubovu wa mabasi.

Huduma hiyo ambayo ilitarajiwa na wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam kuwa mkombozi wa usafiri wa umma kutokana na kujengwa kwa barabara zinazotoa fursa ya kuepuka foleni, imegeuka kuwa kero na aibu wa uwekelezaji mkubwa wa serikali wa kujenga mtandao mkubwa wa barabara za mwendo kasi.

spot_img

Latest articles

Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi yaanza kazi, yakaribisha wananchi kutoa maoni

Na Winfrida Mtoi Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi nchini, imesema tayari imeanza...

Urathi wa Mwalimu Nyerere usaidie kukubali kukosolewa

JUMATATU wiki hii Watanzania walikumbuka kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki...

Nimemsikiliza Gachagua, nikatamani Lowassa 2008 angelipambana vivyo

KWA zaidi ya wiki mbili sasa majirani zetu, Kenya, kumekuwa na siasa za moto....

Kukataa mgombea binafsi ni kukumbatia utumwa

HISTORIA inashuhudia kwamba wapo watumwa walikataa kuwa huru kwa sababu waliamini kwamba pamoja na...

More like this