Uchebe ataja sababu za kurejea Tanzania

Na Winfrida Mtoi

Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Aussems maarufu Ucheba, ametaja sababu ya kurejea kufundisha soka nchini kuwa ni kuvutiwa na mipango ya Singida Black Stars  ambayo amejiunga nayo kwa sasa.

Uchebe ambaye aliipa Simba mafanikio makubwa akichukua mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kuifikisha robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,  amewasili nchini jana Julai Mosi, 2024 na leo kuzungumza na waandishi wa habari kueleza mikakati yake.

Kocha huyo ameeleza kuwa pamoja na kupata ofa nyingi alizikataa baada ya kupigiwa simu na bosi Singida Black Stars  na kumueleza mipango yao, huku akiahidi kuipaisha timu hiyo hadi kufikia mafanikio kama alivyofanya Simba.

“Unapoitaja Tanzania Ulaya watu wanaijua Simba zaidi. Ikumbukwe wakati naichukua  Simba haikuwa katika hali nzuri  lakini niliitengeneza ikawa timu bora yenye mafanikio, hivyo  ndicho kitu ninachotaka kukifanya Singida na malengo  kwa msimu wa 2024/2025 ni kumaliza nafasi ya tatu,” amesema Uchebe.

Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo, Jonathan Kasano, amesema wana malengo ya muda mrefu na mfupi na ndani ya miaka mitatu wanataka kuwa timu ya ushindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amesema wameshafanya usajili kwa asilimia kubwa na walimshirikisha kocha huyo, hivyo ni imani yao watafikia malengo wanahitaji kupitia kocha huyo ambaye ni mzoefu wa kufundisha timu mbalimbali.

spot_img

Latest articles

Tuna deni la kusimamia miradi na kusikiloza kero za wananchi ili kuleta Maendeleo ya kweli: Salome

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa...

2025 mwaka wa mageuzi na matokeo katika mashirika ya umma

Na Mwandishi Wetu MWAKA 2025 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Ofisi ya Msajili wa...

Wakatoliki feki wamechafua hali ya hewa, aibu hii anabeba nani?

TAHARUKI kubwa imeibuka nchini. Unaweza kuiona ukichungulia kwenye mitandao ya kijamii. Imesababishwa na akili...

Mukwala atua Zanzibar, Simba ikiivaa Azam kesho Mapinduzi Cup

Na Winfrida Mtoi WAKATI Simba kitarajia kukabiliana na Azam FC kesho katika mchezo wa nusu...

More like this