Kikokotoo mafao ya Wastaafu sasa asilimia 40

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Serikali imetangaza ongezeko la malipo ya mkupuo kwa wastaafu kutoka asilimia 33 hadi asilimia 40 kwa kundi la watumishi waliokuwa wameshushwa kutoka asilimia 50 hapo awali.

Kwa muda mrefu, wafanyakazi walikuwa wakilalamikia kikokotoo cha pensheni za wastaafu kinachotumika kutokidhi hali halisi ya wanachama, wakitaka kurejeshwa kwa kanuni za zamani zilizotumika kabla ya mwaka 2017.

Msimamo huu mpya umetangazwa, Juni 13, 2024, na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Amesema wastaafu waliokuwa wakipokea asilimia 25 hadi 33 sasa watapandishwa hadi asilimia 35. Pia, walioathirika na mabadiliko ya awali watakuwa sehemu ya mabadiliko haya.

“Serikali imesikia kilio cha watumishi na kufanyia kazi suala la masilahi ya wastaafu, Rais Samia ameelekeza kuongezeka kwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 hadi asilimia 40 kwa kundi la watumishi walioshushwa kutoka asilimia 50 hapo awali.

“Serikali itaendelea kuliangalia kwa karibu suala la masilahi ya wastaafu kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa mifuko yetu,” amesema Dk. Mwigulu.

spot_img

Latest articles

Zawadi ya gari yawapa mzuka mabondia

Na Winfrida Mtoi Waandaaji wa pambano la Dar Boxing Derby wameweka gari aina ya Crown...

Nani anajali kurejesha hadhi Tanzania?

WIKI iliyopita haikuwa ya habari njema kwa Taifa la Tanzania huko duniani. Pamoja na...

TCAA YAIMARISHA HUDUMA KWA WATEJA KUPITIA DAWATI MAALUM

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kupitia kwa Mkurugenzi wake...

TBA YASHINDA TUZO YA BANDA BORA SABASABA, YATANGAZA DIRA YA KUFIKIA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) umeibuka mshindi wa pili na kutunukiwa tuzo...

More like this

Zawadi ya gari yawapa mzuka mabondia

Na Winfrida Mtoi Waandaaji wa pambano la Dar Boxing Derby wameweka gari aina ya Crown...

Nani anajali kurejesha hadhi Tanzania?

WIKI iliyopita haikuwa ya habari njema kwa Taifa la Tanzania huko duniani. Pamoja na...

TCAA YAIMARISHA HUDUMA KWA WATEJA KUPITIA DAWATI MAALUM

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kupitia kwa Mkurugenzi wake...