UVCCM yaukataa mtandao wa X

Na Winfrida Mtoi

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umeishauri Serikali kuchunguza maudhui yaliyomo katika Mtandao wa X (zamani Twitter) kwa kile wanachodai kuwa yanakwenda kinyume na mila na desturi za Watanzania.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Mohammed Kawaida wakati akizungumza na waandishi wa habari Juni 11,2024, jijini Dar es Salaam.

Amesema baadhi ya maudhui yanayotolewa katika mtandao huo yanaweza kusababisha mmomonyoko wa maadili nchini.

“Maudhui ya kingono na mengine si utamaduni wa Mtanzania, umefika wakati sasa kwa Serikali kuufungia mtandao huu kwa sababu hauendani na tamaduni zetu.

“Walianza kwa kutuandaa kisaikolojia wamebadilisha jina kutoka Twitter hadi X ili tuone ni neno la kawaida, watu wengi wanatumia mtandao huu hasa vijana Serikali ichukue hatua kulinda maadili ya vijana na Watanzania wote kwa ujumla,” amesema Kawaida.

Julai 2023 Mmiliki wa mtandao huo, Elon Musk, alitangaza mabadiliko ya nembo yake kutoka ndege hadi herufi X.

spot_img

Latest articles

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

Viongozi wa dini waendelea kihimiza amani uchaguzi mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam VIONGOZI wa dini nchini wameendelea kuhimiza umuhimu wa kudumisha...

More like this