DCEA yaibuka mshindi wa kwanza Tuzo ya uandaaji Bora wa Taarifa za Hesabu 2024/25

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Taasisi za Serikali zinazojitegemea na kutunukiwa Tuzo ya Umahiri wa Uandaaji Bora wa Taarifa za Hesabu kwa mwaka 2024/2025.

Tuzo hiyo inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), inatambua ubora na uzingatiaji wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS) katika uandaaji wa taarifa za hesabu.

Akizungumzia ushindi huo, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema tuzo hiyo ni utambuzi wa ubora, weledi na uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma, na inathibitisha dhamira ya Mamlaka ya kuhakikisha rasilimali inazopatiwa zinasimamiwa kwa uadilifu, uwazi na kuleta tija katika utekelezaji wa majukumu yake ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya.

Amewapongeza na kuwashukuru watumishi wote wa DCEA, hususan Kitengo cha Fedha na Uhasibu pamoja na Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, kwa kujituma na kushirikiana kufanikisha ushindi huo.

DCEA itaendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha, uwazi na uwajibikaji, kwa kuhakikisha kila rasilimali ya umma inatumika kwa ufanisi na kuleta thamani kwa wananchi.

Ushindi huu ni wa mara ya tisa kwa DCEA kupata tuzo za NBAA tangu mwaka 2017ukiakisi dhamira endelevu ya Mamlaka katika kuzingatia viwango na miongozo ya kitaaluma katika usimamizi wa fedha za umma.

spot_img

Latest articles

MIAKA 95 YA KULIANGAZIA TAIFA: TANESCO YAANDIKA HISTORIA MPYA YA NISHATI — MBOSSA

📌 Shirika lafikisha wateja milioni 6 na uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati 4,600. 📌...

WAZIRI HOMERA AIPONGEZA TANESCO KWA MAFANIKIO, IKITIMIZA MIAKA 95

📌Asema imejipanga kuongeza uwezo wa uzalishaji umeme na kufikia megawati 8,000 📌Aeleza Serikali inatambua mchango...

OTR na Newrest zatupia jicho masoko mapya

Na Mwandishi wa OTR Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya kimataifa ya Ufaransa ya huduma za...

Dkt. Yonazi Ahimiza mipango endelevu uimarishaji Mji wa Serikali

Na Mwandishi wetu- Dodoma KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge...

More like this