GBT yaikaribisha BetSasa sokoni, yaitaka kuzingatia maadili

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe ameikaribisha kampuni mpya ya BetSasa na kuitaka kuzingatia maadili na ustawi wa vijana kwa maendeleo ya jamii.

Mbalwe alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampuni ya BetSasa na kampeni ya kuwazawadia wateja wa kampuni hiyo zawadi mbalimbali ikiwemo gari jipya aina ya Jetour.

“Tunawakaribisha BetSasa katika soko la Tanzania, tumeona wameanza vizuri kwa kuja na kampeni hii inayolenga kuwazawadia wateja wao zawadi zenye thamani kubwa ikiwemo gari jipya la kisasa.

“Hata hivyo, tunatoa wito kwao na kampuni nyingine katika sekta hii kuongeza tija ya shughuli zao kwa kuhakikisha wanarejesha kwa jamii kusaidia sekta za afya, elimu, michezo na maeneo mengine muhimu ya maendeleo,” alisema Mbalwe.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa BetSasa, Jimmy Kenneth alisema kampeni hiyo ya mwaka mmoja iitwayo ‘Kusanya Point usepe na Jetour’ inahusisha zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslim.

“Promosheni hii ni mahususi kwa wadau na wateja wa BetSasa hivyo kila wiki zitatoka zawadi mbalimbali na kila baada ya miezi mitatu mshindi mmoja atapata gari jipya aina ya Jetour,” alisema Kenneth.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu huyo, BetSasa imejipanga kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia Sheria, kanuni, masharti, taratibu na muongozo ya mamlaka zinazosimamia michezo ya kubahatisha na kutekeleza wajibu wake kwa jamii.

spot_img

Latest articles

DKT. YONAZI AHIMIZA UIMARISHWAJI WA MIFUMO YA KITAASISI YA UFUATILIAJI NA TATHMINI NCHINI

Na Mwandishi Wetu- Morogoro. KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge Uratibu na Wenye...

OTR, Benki ya Dunia zajadili fursa za uwekezaji katika taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) na Benki ya Dunia zimeonesha nia...

Mkutano wa Kimataifa wa Sekta ya Madini kukutanisha washiriki zaidi ya 1,700

Na Tatu Mohamed MKUTANO wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini (TMIC...

WAANDISHI 64 WAFUZU TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026

Na Tatu Mohamed JUMLA ya Waandishi wa Habari 64 na vyombo vya habari 11 vimefuzu...

More like this