OTR, Benki ya Dunia zajadili fursa za uwekezaji katika taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu

OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) na Benki ya Dunia zimeonesha nia ya kuimarisha ushirikiano katika kuboresha utendaji wa taasisi za umma na kufungua fursa zaidi za uwekezaji wa sekta binafsi, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono utekelezaji wa Dira 2050.

Hayo yalijadiliwa Jumanne, Novemba 17, 2026, katika kikao kati ya Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, na ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Mkurugenzi wa Benki hiyo anayesimamia Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe, Bw. Firas Raad, uliofika OTR kwa ziara ya kikazi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mchechu alisema utendaji imara wa taasisi na kampuni zinazomilikiwa na Serikali ni muhimu katika kufanikisha malengo ya Dira 2050, inayolenga kuifanya sekta binafsi ichangie asilimia 70 ya uchumi, huku sekta ya umma ikichangia asilimia 30.

Alieleza kuwa ili kuvutia mitaji binafsi, taasisi hizo zinapaswa kuimarisha mifumo ya utawala bora, kuongeza ufanisi wa kifedha na kuandaa miradi yenye tija na inayoweza kuvutia wawekezaji.

Alibainisha kuwa tangu mwaka 2023, OTR imekuwa ikitekeleza mageuzi yanayolenga kuimarisha usimamizi wa utendaji, uwajibikaji wa viongozi na ufanisi wa taasisi hizo.

Mageuzi hayo yanajumuisha mfumo wa upimaji utendaji unaozingatia maeneo matano: matokeo ya kifedha, malengo ya kisekta, utawala bora, kuridhika kwa wateja na utendaji wa watumishi.

Mchechu alihimiza Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), ambalo ni sehemu ya Benki ya Dunia inayojikita katika uwekezaji wa sekta binafsi, kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika kampuni za umma zinazoendeshwa kibiashara, akisisitiza kuwa umiliki wa Serikali haupaswi kuwa kikwazo kwa kampuni hizo kupata mitaji binafsi.

Kwa upande wake, Raad alisifu mageuzi yanayotekelezwa na OTR, hususan katika kuimarisha utawala bora, upimaji wa utendaji na utoaji huduma. Alisema taasisi za umma zenye mifumo imara ya uendeshaji na uwezo mzuri wa kifedha zina nafasi kubwa zaidi ya kuvutia mitaji binafsi.

Alieleza kuwa Benki ya Dunia tayari imeweka dhamira ya ufadhili inayozidi $8 bilioni katika sekta mbalimbali nchini. Aliongeza kuwa benki hiyo inaendelea kutumia rasilimali zake za maendeleo kuchochea uwekezaji zaidi katika sekta binafsi, hususan katika sekta za nishati, usafiri na maendeleo ya miji.

Pande hizo mbili zilikubaliana kuendeleza mazungumzo ili kubaini maeneo mahsusi ya ushirikiano, yakiwemo fursa za uwekezaji, uandaaji wa miradi inayokidhi vigezo vya ufadhili na uendelezaji wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi.

spot_img

Latest articles

Mkutano wa Kimataifa wa Sekta ya Madini kukutanisha washiriki zaidi ya 1,700

Na Tatu Mohamed MKUTANO wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini (TMIC...

WAANDISHI 64 WAFUZU TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026

Na Tatu Mohamed JUMLA ya Waandishi wa Habari 64 na vyombo vya habari 11 vimefuzu...

MIRADI YA UMEME KUIMARISHA GRIDI YA TAIFA NA KUCHOCHEA UKUAJI WA FURSA ZA KIJAMII NA KIUCHUMI– WAZIRI HOMERA

📌MD Twange atoa taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa Miradi ya kuimarisha Gridi ya...

Ndejembi ahimiza nishati safi, Lake Ges na Mama Salma wagawa mitungi ya kupikia

Na Mwandishi Wetu, Mchinga MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi,...

More like this

Mkutano wa Kimataifa wa Sekta ya Madini kukutanisha washiriki zaidi ya 1,700

Na Tatu Mohamed MKUTANO wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini (TMIC...

WAANDISHI 64 WAFUZU TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026

Na Tatu Mohamed JUMLA ya Waandishi wa Habari 64 na vyombo vya habari 11 vimefuzu...

MIRADI YA UMEME KUIMARISHA GRIDI YA TAIFA NA KUCHOCHEA UKUAJI WA FURSA ZA KIJAMII NA KIUCHUMI– WAZIRI HOMERA

📌MD Twange atoa taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa Miradi ya kuimarisha Gridi ya...