DKT. YONAZI AHIMIZA UIMARISHWAJI WA MIFUMO YA KITAASISI YA UFUATILIAJI NA TATHMINI NCHINI

Na Mwandishi Wetu- Morogoro.

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. Jim Yonazi amehimiza watendaji wa serikali kuendelea kuimarisha mifumo ya kitaasisi ya Ufuatiliaji na tathimini sambamba na ushirikiano wa kazi katika hatua za mipango ya bajeti.

Kauli Hiyo ameitoa Mkoani Morogoro leo tarehe 17 Novemba, 2026 wakati akifungua mafunzo ya kimkakati ya uongozi katika ufuatiliaji na tathimini yaliyohusisha Wakurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathimini, Wakurugenzi wa Mipango wa wizara, Wakurugenzi kutoka Serikali za Mikoa.

Ameongeza kusema hatua hiyo itasaidia katika kuimarisha kutambua mahitajia ya tathimini na kusimamia tathimini zinajibu maswali muhimu katika utekelezaji wa shughuli za serikali, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mawasiliano yenye Ushahidi kwa ajili ya kufanya maamuzi ya kimkakati wa viongozi wetu.

“Maamuzi ambayo yataleta mabadiliko na kuharakisha mafanikio kwa wananchi wetu huku tukizingatia uimarishwaji wa matumizi ya mifumo ya TEHAMA na kuzingatia umuhimu wa kujifunza uwajibikaji na kuchukua hatua kuboresha utendaji,”alieleza Dkt. Yonazi.

Aliongezea kuwa upo umuhimu wa mafunzo hayo ili kuhakikisha maarifa yanayopatikana yanatutoa kutoka hatua moja kwenda nyingine endapo yatatumika ipasavyo na kuleta maana zaidi kwa jamii.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Sakina Mwinyimkuu, amesema kuwa mafunzo hayo kwa viongozi ni muhimu katika kuimarisha usimamizi wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathmini, hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Mafunzo haya, yanatarajiwa kuendelea kufanyika kila mwaka, ili kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika usimamizi wa mipango, ufuatiliaji wa utekelezaji wake pamoja na tathmini ya matokeo, katika kuongeza ufanisi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa ujumla,” alieleza.

Bi. Mwinyimkuu ameishukuru Taasisi ya Uongozi kwa kuratibu mafunzo hayo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, akieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa viongozi na wataalamu katika eneo la Ufuatiliaji na Tathmini.

Kwa upande Bw, Gerald Peter Sondo Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathimini Jiji la Dar es Salaam, amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha ushirikiano na unganishaji wa sekta kupitia matumizi ya takwimu na ushahidi katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo.

“Mafunzo yametuwezesha washiriki kujikita katika matumizi ya ufanisi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ikiwemo matumizi ya Akili Unde (AI) katika kuchambua, kuandaa na kuchakata taarifa mbalimbali kwa weledi na kwa muda mfupi,” alibainisha.

Bw. Sondo amehimiza kuongeza umakini kwa taarifa zinazozalishwa au kuchakatwa kwa kutumia AI kwa kufanya uhakiki wa kina kabla ya kutolewa kwa umma.

spot_img

Latest articles

OTR, Benki ya Dunia zajadili fursa za uwekezaji katika taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) na Benki ya Dunia zimeonesha nia...

Mkutano wa Kimataifa wa Sekta ya Madini kukutanisha washiriki zaidi ya 1,700

Na Tatu Mohamed MKUTANO wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini (TMIC...

WAANDISHI 64 WAFUZU TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026

Na Tatu Mohamed JUMLA ya Waandishi wa Habari 64 na vyombo vya habari 11 vimefuzu...

MIRADI YA UMEME KUIMARISHA GRIDI YA TAIFA NA KUCHOCHEA UKUAJI WA FURSA ZA KIJAMII NA KIUCHUMI– WAZIRI HOMERA

📌MD Twange atoa taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa Miradi ya kuimarisha Gridi ya...

More like this

OTR, Benki ya Dunia zajadili fursa za uwekezaji katika taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) na Benki ya Dunia zimeonesha nia...

Mkutano wa Kimataifa wa Sekta ya Madini kukutanisha washiriki zaidi ya 1,700

Na Tatu Mohamed MKUTANO wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini (TMIC...

WAANDISHI 64 WAFUZU TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026

Na Tatu Mohamed JUMLA ya Waandishi wa Habari 64 na vyombo vya habari 11 vimefuzu...