Utafiti: Joto kali linaongeza hatari kujifungua mtoto mfu

Kufanya kazi kwenye joto kali kunaweza kuongeza hatari ya kuzaliwa mtoto mfu na kuharibika kwa mimba kwa wanawake wajawazito, kulingana na utafiti mpya uliofanyika nchini India.

Utafiti huo uligundua kuwa hatari kwa mama anayetarajia kujifungua ni kubwa zaidi kuliko ilivyofikiriwa hapo awali.

Wanawake mia nane wajawazito katika jimbo la kusini mwa India la Tamil Nadu walishiriki katika utafiti huo, ambao ulianzishwa mwaka 2017 na taasisi ya Sri Ramachandra Institute of Higher Education and Research (SRIHER).

Kakriban nusu ya wale walioshiriki walikuwa ni wafanyakazi ambao wanakabiliwa na viwango vya juu vya joto, kama katika kilimo, ufyatuaji wa matofali na kutengeneza chumvi.

”Wanawake wajawazito nchini India wako mstari wa mbele katika kukabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi,” anasema Prof Hirst. Wastani wa halijoto la dunia inakadiriwa kuongezeka kwa karibu digrii tatu mwishoni mwa karne hii, ikilinganishwa na nyakati za kabla ya viwanda.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linaonya juu ya tishio hilo kwa watu wote, lakini wanawake wajawazito wakikabiliwa na madhara makubwa zaidi.

Kwa sasa hakuna ushauri rasmi wa kimataifa kwa wanawake wajawazito wanaofanya kazi katika maeneo yenye joto. Hata hivyo Prof. Hirst anasema wanawake wajawazito wanaofanya kazi kwenye joto wanaweza kujilinda kwa kuepuka kukaa juani kwa muda mrefu, kupumzika kwa kukaa kivulini, kuepuka kuchomwa na jua kwa muda mrefu na kunywa maji mengi.

Tafiti za awali zilifanywa katika nchi zenye mapato ya juu kama vile Marekani na Australia zimeonyesha kuhusu ongezeko la asilimia 15 la hatari ya mtoto kuzaliwa kabla ya wakati na kuzaa mtoto aliyekufa wakati wa joto kali.

”Matokeo ya hivi karibuni kutoka India ni ya kutisha na yanatia wasiwasi,” anasema Prof Hirst, ”na yana maana pana zaidi.”

Mwongozo ambao upo kwa ajili ya kufanya kazi katika hali ya hewa ya joto, unatokana na tafiti zilizohusisha mwanajeshi wa Marekani katika miaka ya 1960 na 70, akiwa na uzito wa 70-75kg na 20% ya mafuta ya mwili.

Kiwango Cha juu Cha joto salama Kwa watu wanaofanya kazi NZITO ni 27.5c kulingana na Taasisi ya usalama na afya kazini ya Marekani.

Chanzo: Bbc Swahili

spot_img

Latest articles

Kapinga azindua Kituo Mama cha gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) DAR

📌 Ni cha Pili kwa ukubwa barani Afrika, Cha Kwanza kwa ukubwa EAC 📌 Kujaza...

Mapato yasiyo ya kodi yafikia asilimia 67, OMH yadhamiria kufikia lengo la mwaka

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), imeendelea kuonesha mafanikio...

Dkt. Biteko: Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kufikia asilimia 75 mwaka 2030

Na Mwandishi Wetu 📌 Dkt. Biteko akutana na Balozi wa Japan nchini 📌 Tanzania na...

Twange aanza kazi rasmi Tanesco

📌Aomba ushirikiano ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na umeme wa uhakika. 📌Aahidi Kuendeleza Mazuri yaliyofanyika...

More like this

Kapinga azindua Kituo Mama cha gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) DAR

📌 Ni cha Pili kwa ukubwa barani Afrika, Cha Kwanza kwa ukubwa EAC 📌 Kujaza...

Mapato yasiyo ya kodi yafikia asilimia 67, OMH yadhamiria kufikia lengo la mwaka

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), imeendelea kuonesha mafanikio...

Dkt. Biteko: Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kufikia asilimia 75 mwaka 2030

Na Mwandishi Wetu 📌 Dkt. Biteko akutana na Balozi wa Japan nchini 📌 Tanzania na...