TANZANIA YATUMIA MKUTANO MKUU WA ISA INDIA KUVUTIA UWEKEZAJI WA NISHATI JUA KUFIKIA MALENGO YA DIRA 2050

📌Hatua zinazochukuliwa na Serikali kupunguza gharama za awali za uwekezaji zaelezwa

Na Mwandishi Wetu

TANZANIA imetumia Mkutano Mkuu wa Tisa wa Muungano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (International Solar Alliance – ISA) unaofanyika nchini India, kueleza maeneo yanayohitaji ushirikiano katika uendelezaji wa nishati jua ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza uzalishaji wa umeme na kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Akizungumza tarehe 03 Novemba 2026 katika Mkutano huo unaohusisha nchi wanachama na Washirika wa Maendeleo zaidi ya 125, Mwakilishi wa Tanzania katika ISA, Bw.Emilian Nyanda kutoka Wizara ya Nishati amesema Serikali imeweka mkazo katika kuendeleza nishati jadidifu, hususan nishati ya jua, ili kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuchochea shughuli za kiuchumi na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ameeleza kuwa, kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Tanzania inalenga kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme kutoka gigawati 4.6 za sasa hadi gigawati 8 ifikapo mwaka 2030 na gigawati 70 mwaka 2050, huku nishati ya jua ikitarajiwa kuwa miongoni mwa vyanzo muhimu vya kufanikisha malengo hayo.,

Katika hatua nyingine amesema Tanzania inapiga hatua katika uzalishaji wa umeme wa jua kupitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Kishapu mkoani Shinyanga wenye uwezo wa kuzalisha megawati 150, ambapo awamu ya kwanza ya megawati 50 imekamilika na awamu ya pili ya megawati 100 ipo katika hatua za utekelezaji.

Ameongeza kuwa,kwa sasa megawati 100 za umeme jua zinaingia katika gridi ya Taifa huku Serikali ikilenga kuongeza megawati 1,000 za umeme huo wa jua ifikapo mwaka 2035 kupitia uwekezaji wa sekta ya umma na binafsi.

Amesema Wizara ya Nishati kwa kushirkiana na TANESCO imeendelea na jitihada za kutambua na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya uwekezaji wa miradi ya nishati ya jua, kufanya tafiti za upembuzi yakinifu na tathmini za athari kwa mazingira, hatua inayolenga kupunguza gharama za awali za uwekezaji na kuvutia wawekezaji zaidi nchini.

Kuhusu usambazaji wa umeme jua, amesema, pamoja na kuongeza mchango wake kwenye gridi ya taifa, Tanzania inaendelea kutumia teknolojia ya nishati hiyo kufikisha huduma katika maeneo ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa, ikiwemo visiwa vilivyopo katika maziwa makuu na Bahari ya Hindi.

Nishati hiyo pia inatumika katika shughuli za uzalishaji mali zikiwemo kilimo, umwagiliaji, usindikaji wa mazao, uvuvi, ufugaji na usambazaji wa maji.

Nyanda amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na ISA ambao umewezesha kuanzishwa kwa Kituo cha Umahiri cha Mafunzo ya Teknolojia ya Nishati ya Jua (Solar Technology Application Centre – STAR-C) katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kinachotoa mafunzo kwa wataalamu wa ndani, huku Watanzania wengine wakinufaika na mafunzo ya kitaalamu katika taasisi mbalimbali za kimataifa.

Amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa ISA, sekta binafsi na washirika wa maendeleo katika kuvutia mitaji, teknolojia na utaalamu ili kuharakisha utekelezaji wa miradi ya nishati jadidifu na kufanikisha azma ya Serikali ya kujenga uchumi imara na endelevu kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Mkutano huo umefunguliwa leo na Waziri anayeshughulikia masuala ya Nishati Jadidifu wa India, Shri Pralhad Joshi ambaye ndiye anayeongoza Mkutano Mkuu wa 9 wa ISA.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Joshi amesisitiza umuhimu wa mataifa yote kushirikiana ili kufanya nishati ya jua ipatikane kwa bei nafuu duniani kote, pia ametoa wito wa kuongeza uwekezaji kwenye nishati safi, hasa katika nchi zinazoendelea, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kukuza maendeleo endelevu.

spot_img

Latest articles

UCSAF YAPELEKA HUDUMA ZA MAWASILIANO KWA WANANCHI ZAIDI YA MILIONI 8

Na Tatu Mohamed WANANCHI wapatao milioni 8.5 wamepata huduma za mawasiliano kupitia mradi wa ujenzi...

NECTA YAFUTA MATOKEO YA WATAHINIWA 31 WA DARASA LA SABA

Na Tatu Mohamed BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 31 wa...

MATENGENEZO YA BOMBA KUU KUPUNGUZA MAJI KWA SIKU NNE DAR NA PWANI

Na Mwandishi Wetu ‎‎WAKAZI wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wanatarajiwa kukabiliwa na...

MEENA ACHAGULIWA TENA KUWA MWENYEKITI WA RUJAT

Na Tatu Mohamed, Dodoma WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini...

More like this

UCSAF YAPELEKA HUDUMA ZA MAWASILIANO KWA WANANCHI ZAIDI YA MILIONI 8

Na Tatu Mohamed WANANCHI wapatao milioni 8.5 wamepata huduma za mawasiliano kupitia mradi wa ujenzi...

NECTA YAFUTA MATOKEO YA WATAHINIWA 31 WA DARASA LA SABA

Na Tatu Mohamed BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 31 wa...

MATENGENEZO YA BOMBA KUU KUPUNGUZA MAJI KWA SIKU NNE DAR NA PWANI

Na Mwandishi Wetu ‎‎WAKAZI wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wanatarajiwa kukabiliwa na...