MEENA ACHAGULIWA TENA KUWA MWENYEKITI WA RUJAT

Na Tatu Mohamed, Dodoma

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT), wamemchagua tena Mwanahabari Nguli na Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Media Brains, Neville Meena, kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa kipindi kingine cha miaka minne.

Meena ametangazwa mshindi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Felix Mwakyembe, baada ya kupata kura 74 kati ya 77 zilizopigwa, akiwaacha nyuma wagombea wenzake wawili, Meshack Ngumba na Andrea Ngolola, waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Uchaguzi huo umefanyika jana Oktoba 31, 2026, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, jijini Dodoma, ambapo wanachama walichagua viongozi watakaosimamia chama hicho kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Meena ambaye pia amewahi kuwa Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na ni miongoni mwa waasisi wa RUJAT, amesema kura nyingi alizopata ni dhamana anayopaswa kuilipa kwa kuwatumikia wanachama kwa moyo wake wote.

Amesema atahakikisha anasimamia malengo ya RUJAT, ikiwamo kuhakikisha habari zinazohusu wananchi wa vijijini zinapewa kipaumbele katika vyombo vya habari ili changamoto na fursa zinazowakabili zipate nafasi ya kuwasilishwa kwa jamii na mamlaka husika.

Ameongeza kuwa kipaumbele kingine ni kukijengea uwezo chama hicho na kuimarisha ujuzi wa waandishi wa habari katika kuandaa na kuandika habari zinazogusa maslahi ya umma, akieleza kuwa atashirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha RUJAT inapiga hatua katika utekelezaji wa majukumu yake.

Katika uchaguzi huo, Hamida Ramadhan kutoka mkoani Dodoma amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, huku Prosper Kwigize kutoka Kasulu mkoani Kigoma akichaguliwa tena kuwa Katibu kwa kupata kura 76 kati ya 77 zilizopigwa.

Kwa upande mwingine, Zena Chitwanga amechaguliwa kuwa Mweka Hazina wa RUJAT, huku wajumbe saba waliochaguliwa kuunda Kamati Tendaji wakiwa Musa Siwayombe, Devotha Paul, Malunde Kadama, Rashid Mtagaluka, Anne Robi, Andrea Ngolola na Fadhili Mwangamola.

Kwa mujibu wa mabadiliko ya Katiba yaliyopitishwa na wanachama wa RUJAT, uongozi mpya wa Meena na viongozi wenzake utadumu kwa kipindi cha miaka minne kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine.

spot_img

Latest articles

WAZIRI MAVUNDE ASHUHUDIA MKOPO WA BILIONI 50 KWA WACHIMBAJI WADOGO SONGWE

▪️Ni kwa ajili ya mtaji, mitambo na CIP ▪️Atoa leseni kwa vikundi 118 kupitia Mradi...

MSIGWA ATAKA HABARI ZA VIJIJINI KUPEWA KIPAUMBELE

Na Tatu Mohamed KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson...

MKUU WA WILAYA YA LUDEWA AWATAKA VIONGOZI KUWA MABALOZI WA ELIMU YA FEDHA NCHINI

Na Mwandishi wetu, Njombe MKUU wa Wilaya ya Ludewa, Olivanus Thomas, 8amewahimiza viongozi wa wilaya...

NeST yawezesha Zabuni za Sh Trilioni 42.6, serikali yaokoa Sh. Bilioni 28

Na Tatu Mohamed MFUMO wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) umewezesha kutolewa kwa zabuni...

More like this

WAZIRI MAVUNDE ASHUHUDIA MKOPO WA BILIONI 50 KWA WACHIMBAJI WADOGO SONGWE

▪️Ni kwa ajili ya mtaji, mitambo na CIP ▪️Atoa leseni kwa vikundi 118 kupitia Mradi...

MSIGWA ATAKA HABARI ZA VIJIJINI KUPEWA KIPAUMBELE

Na Tatu Mohamed KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson...

MKUU WA WILAYA YA LUDEWA AWATAKA VIONGOZI KUWA MABALOZI WA ELIMU YA FEDHA NCHINI

Na Mwandishi wetu, Njombe MKUU wa Wilaya ya Ludewa, Olivanus Thomas, 8amewahimiza viongozi wa wilaya...