NECTA YAFUTA MATOKEO YA WATAHINIWA 31 WA DARASA LA SABA

Na Tatu Mohamed

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 31 wa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) mwaka 2026 ambapo kati ya hao 26 walibainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani na watano waliandika lugha ya matusi katika skripti zao.

Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo leo Novemba 3, 2026, Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed, amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 5(2)(i) na (j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani Sura ya 107 pamoja na kifungu cha 30(2)(b) cha Kanuni za Mitihani za mwaka 2016.

Aidha, amesema Baraza limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 371 walioshindwa kufanya mtihani kwa idadi kubwa ya masomo au masomo yote, na kuwapa fursa ya kurudia mtihani huo mwaka 2027 kwa mujibu wa kifungu cha 32(1) cha Kanuni za Mitihani.

Hata hivyo amesema ufaulu wa Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi umeongezeka kwa asilimia 3.42, kutoka asilimia 81.80 mwaka 2025 hadi asilimia 85.22 mwaka 2026, huku watahiniwa 970,876 wakifaulu kati ya 1,139,273 waliofanya mtihani huo uliofanyika Septemba mwaka huu.

“Watahiniwa 429,667 sawa na asilimia 37.72 wamepata madaraja ya A na B, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.82 ikilinganishwa na mwaka 2025. Kwa upande wa wasichana, ufaulu katika madaraja hayo umeongezeka kutoka asilimia 33.71 mwaka 2025 hadi asilimia 34.27 mwaka 2026, huku wavulana ukipanda kutoka asilimia 40.73 hadi asilimia 41.90,” amesema.

Ameongeza kuwa ufaulu wa jumla kwa wasichana umefikia asilimia 86.18 baada ya watahiniwa 527,622 kufaulu, huku wavulana 443,254 wakifaulu kwa asilimia 84.43.

“Ufaulu wa wasichana umeongezeka kwa asilimia 3.22 na wavulana kwa asilimia 3.67 ikilinganishwa na mwaka 2025” amefafanua.

Amebainisha kuwa shule 20,010 zilifanya mtihani huo, ambapo shule 12,914 sawa na asilimia 64.54 zimepata wastani wa daraja C, huku shule 5,670 sawa na asilimia 28.33 zikipata wastani wa madaraja A na B ambapo kwa ujumla, shule 18,584 sawa na asilimia 92.87 zimepata wastani wa madaraja A hadi C.

“Kwa upande wa masomo, Kiswahili kimeongoza kwa ufaulu wa asilimia 93.13, kikifuatiwa na Uraia na Maadili kwa asilimia 90.12, Sayansi na Teknolojia asilimia 80.34, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi asilimia 76.53, Hisabati asilimia 62.56 na Kiingereza asilimia 50.50.

“Ufaulu wa somo la Kiswahili umeongezeka kwa asilimia 5.56 ikilinganishwa na mwaka 2025, huku Kiingereza ukiongezeka kwa asilimia 0.39. Hata hivyo, ufaulu wa Sayansi na Teknolojia umeshuka kwa asilimia 4.09 kutoka asilimia 84.43 mwaka 2025 hadi asilimia 80.34 mwaka 2026,” amesema.

Kwa mwaka 2026, jumla ya watahiniwa 1,168,718 walisajiliwa kufanya mtihani huo, wakiwemo wasichana 637,214 sawa na asilimia 54.52 na wavulana 531,504 sawa na asilimia 45.48. Kati yao, watahiniwa 1,139,318 walifanya mtihani huo, sawa na asilimia 97.48 ya waliosajiliwa.

spot_img

Latest articles

MATENGENEZO YA BOMBA KUU KUPUNGUZA MAJI KWA SIKU NNE DAR NA PWANI

Na Mwandishi Wetu ‎‎WAKAZI wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wanatarajiwa kukabiliwa na...

MEENA ACHAGULIWA TENA KUWA MWENYEKITI WA RUJAT

Na Tatu Mohamed, Dodoma WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini...

WAZIRI MAVUNDE ASHUHUDIA MKOPO WA BILIONI 50 KWA WACHIMBAJI WADOGO SONGWE

▪️Ni kwa ajili ya mtaji, mitambo na CIP ▪️Atoa leseni kwa vikundi 118 kupitia Mradi...

MSIGWA ATAKA HABARI ZA VIJIJINI KUPEWA KIPAUMBELE

Na Tatu Mohamed KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson...

More like this

MATENGENEZO YA BOMBA KUU KUPUNGUZA MAJI KWA SIKU NNE DAR NA PWANI

Na Mwandishi Wetu ‎‎WAKAZI wa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wanatarajiwa kukabiliwa na...

MEENA ACHAGULIWA TENA KUWA MWENYEKITI WA RUJAT

Na Tatu Mohamed, Dodoma WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini...

WAZIRI MAVUNDE ASHUHUDIA MKOPO WA BILIONI 50 KWA WACHIMBAJI WADOGO SONGWE

▪️Ni kwa ajili ya mtaji, mitambo na CIP ▪️Atoa leseni kwa vikundi 118 kupitia Mradi...