Tanzania kuandika historia leo, Rais Samia kuzindua Bwawa la Julius Nyerere

Na Tatu Mohamed

TANZANIA inaandika ukurasa mpya katika historia ya sekta ya nishati leo Agosti 22, 2026, wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), mradi mkubwa wa kimkakati unaotarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini.

Uzinduzi huo unafanyika baada ya kukamilika kwa mitambo yote tisa ya mradi huo yenye uwezo wa kuzalisha jumla ya Megawati 2,115, hatua inayotarajiwa kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa matumizi ya wananchi, shughuli za uzalishaji na uwekezaji.

Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere umegharimu takribani Shilingi trilioni 7.452, huku ukifadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati inayolenga kuimarisha uchumi wa taifa.

Kukamilika kwa mradi huo kunatajwa kuwa hatua muhimu katika safari ya Tanzania ya kuongeza uzalishaji wa umeme na kuweka mazingira bora kwa maendeleo ya viwanda, biashara na shughuli nyingine za kiuchumi zinazohitaji nishati ya uhakika.

Bwawa hilo pia lina umuhimu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kuifanya nishati kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi, maendeleo ya viwanda, uwekezaji, ubunifu na ustawi wa wananchi, huku uzinduzi wa leo ukiwa kilele cha safari ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kitaifa.

spot_img

Latest articles

DAWASA YAPELEKA TABASAMU KUNDI MAALUM WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imehitimisha wiki ya...

TANESCO YANG’ARA TUZO ZA UMAHIRI WA MAWASILIANO KWA UMMA

📌 Yanyakua tuzo nne katika vipengele mbalimbali 📌 Yatambuliwa kwa ubora katika mawasiliano ya kimkakati,...

BRELA YAFUNGUA FURSA YA URASIMISHAJI KWA WADAU WA UCHUMI WA UBUNIFU ARUSHA

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeweka kambi ya...

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM SOMBI ATEMBELEA KIKUNDI CHA UKOMBOZI WA VIJANA KALAMBO

Na Mwandishi Wetu IKIWA ni sehemu ya shughuli za Wiki ya UVCCM 2026, Makamu...

More like this