PBPA: Tanzania yazidi kuwa kitovu cha usambazaji wa mafuta Afrika Mashariki na Kati

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAKALA wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) umesema mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja umeifanya Tanzania kuendelea kuwa kitovu muhimu cha usambazaji wa mafuta kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, hatua inayochochea biashara ya kikanda na kuongeza mchango wa sekta ya nishati katika uchumi wa taifa.

Akizungumza katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima ‘Nanenane’ yanayoendelea jijini Dodoma, Mhandisi wa Petroli wa PBPA, Rehema Mahundi, amesema mbali na kuhakikisha mafuta yanapatikana kwa uhakika nchini, wakala huo umewezesha pia nchi jirani kunufaika na miundombinu ya bandari za Tanzania.

“Kupitia mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja, Tanzania siyo tu inahudumia mahitaji yake ya ndani, bali pia inatoa huduma kwa nchi jirani kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda, Malawi na Zambia. Hii inaifanya nchi kuwa kitovu muhimu cha biashara ya mafuta katika ukanda wetu,” amesema Mahundi.

Amesema PBPA husimamia mchakato mzima wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja kupitia zabuni za kimataifa zinazofanyika kila mwezi, ambapo mikataba huandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya mafuta ya miezi miwili ijayo.Kwa mujibu wa Mahundi, utaratibu huo umeondoa changamoto za upatikanaji wa mafuta na kuifanya Serikali kuwa na uwezo wa kupanga mahitaji ya nchi kwa ufanisi zaidi.

“Tunapanga uagizaji mapema kulingana na mahitaji halisi ya soko. Hii inahakikisha mafuta yanapatikana wakati wote na shughuli za uzalishaji, usafirishaji na biashara haziathiriki,” amesema.

Ameeleza kuwa mfumo huo umeongeza uwazi katika sekta ya mafuta kwa kuwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za mafuta yaliyopo nchini, yanayoingia na yanayotarajiwa kuwasili, jambo linalorahisisha usimamizi wa sekta hiyo.

Amesema upatikanaji wa mafuta kwa uhakika ni nguzo muhimu ya maendeleo ya sekta mbalimbali za uchumi, zikiwemo viwanda, kilimo, usafirishaji na utalii, ambazo zinategemea nishati hiyo kuendesha shughuli zake.

Ameongeza kuwa PBPA itaendelea kuboresha mfumo wa uagizaji wa mafuta ili kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa lango la uhakika la usambazaji wa mafuta katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, sambamba na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Aidha, amewataka wananchi kutembelea banda la PBPA katika Maonesho ya Nanenane ili kupata elimu kuhusu majukumu ya wakala huo na namna mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja unavyochangia maendeleo ya uchumi wa Tanzania na nchi jirani.

spot_img

Latest articles

UDOM yabuni mfumo wa kidijitali wa kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna

Na Mwandishi Wetu CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimebuni mfumo wa kidijitali unaowezesha wakulima kufuatilia...

ZSTC yapongeza mchango wa TADB katika kukuza sekta ya karafuu Zanzibar

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) limesema ushirikiano wake na...

Mikopo ya TADB yaongeza nguvu biashara ya parachichi, Eatfresh yawahakikishia wakulima soko

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Eatfresh (GBRI Business Solutions) imesema ufadhili wa zaidi ya Sh...

GST: Tafiti za Jiosayansi ni Nguzo ya Dira ya Taifa 2050 na Uchumi Endelevu wa Madini

Na Mwandishi Wetu, Dodoma MWENYEKITI wa Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini...

More like this

UDOM yabuni mfumo wa kidijitali wa kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna

Na Mwandishi Wetu CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimebuni mfumo wa kidijitali unaowezesha wakulima kufuatilia...

ZSTC yapongeza mchango wa TADB katika kukuza sekta ya karafuu Zanzibar

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) limesema ushirikiano wake na...

Mikopo ya TADB yaongeza nguvu biashara ya parachichi, Eatfresh yawahakikishia wakulima soko

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Eatfresh (GBRI Business Solutions) imesema ufadhili wa zaidi ya Sh...