NIC: Waandishi wa habari vinara wa kuhamasisha matumizi ya bima

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC Insurance) limewapongeza waandishi wa habari kwa kujitokeza kwa wingi kukata bima za maisha na mali katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima ‘Nanenane’ yanayoendelea jijini Dodoma, likisema hatua hiyo ni ishara ya kuongezeka kwa uelewa kuhusu umuhimu wa bima na mfano unaopaswa kuigwa na wananchi.

Akizungumza katika maonesho hayo, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC Insurance, Karimu Meshack, amesema ndani ya siku moja waandishi wa habari 11 walikata bima mbalimbali, ikiwemo bima za maisha na mali, jambo alilosema linaonyesha mabadiliko chanya ya mtazamo kuhusu umuhimu wa kujilinda dhidi ya majanga yasiyotabirika.

Amesema waandishi wa habari ni wadau muhimu katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya maendeleo, hivyo wanapochukua hatua ya kujikinga kwa bima wanakuwa mabalozi wa vitendo wanaoweza kuhamasisha wananchi kufanya maamuzi sahihi kuhusu usalama wa maisha na mali zao.

“Kwa muda mrefu waandishi wamekuwa mstari wa mbele kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa bima. Leo tunafurahia kuona nao wanachukua hatua ya kutumia huduma hizi, jambo linalowapa uhalisia zaidi wanapowahamasisha wengine,” amesema.

Amebainisha kuwa taaluma ya uandishi wa habari ina changamoto na mazingira yenye vihatarishi mbalimbali, hivyo ni muhimu kwa waandishi kuwa na kinga ya kifedha itakayowalinda wao na familia zao endapo yatatokea majanga yasiyotarajiwa.

Amesema ongezeko la waandishi wa habari wanaojiunga na huduma za bima linaunga mkono jitihada za Serikali za kuongeza matumizi ya bima nchini na kujenga jamii yenye uwezo wa kukabiliana na athari za majanga bila kuyumbisha uchumi wa familia.

Hata hivyo amewataka waandishi wengine nchini kuiga mfano huo kwa kutambua kuwa pamoja na wajibu wao wa kuhabarisha umma, pia wana wajibu wa kulinda ustawi wa familia zao kupitia huduma za bima.

Amesisitiza kuwa bima si huduma inayopaswa kuzingatiwa baada ya janga kutokea, bali ni uwekezaji wa mapema unaowapa wananchi utulivu wa kifedha na uhakika wa kuendelea na maisha pale wanapokumbana na changamoto zisizotarajiwa.

Ametoa wito kwa wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nanenane kutumia fursa hiyo kutembelea banda la NIC Insurance na kupata elimu kuhusu aina mbalimbali za bima zinazotolewa, ili waweze kuchagua huduma zinazokidhi mahitaji yao na kujenga kinga ya maisha na mali zao.

Baadhi ya waandishi waliokata bima katika maonesho hayo walisema wamechukua uamuzi huo ili kuhakikisha familia zao zinapata ulinzi wa kifedha endapo watapatwa na majanga, huku wengine wakieleza kuwa wamekata bima za nyumba na mali ili kulinda vitega uchumi walivyovijenga kwa muda mrefu.

spot_img

Latest articles

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...

MRADI WA UMEME SIMIYU KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WANANCHI

📌 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...

More like this

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...