DAWASA MTAA KWA MTAA KUTATUA CHANGAMOTO ZA HUDUMA

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Wilaya ya Ubungo imeanza utekelezaji wa mpango wa kuboresha huduma ya maji katika Mtaa wa Kimara B kwa kulaza bomba lenye uwezo mkubwa zaidi, hatua inayolenga kukidhi mahitaji ya sasa ya wakazi na kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji iliyodumu kwa muda mrefu.

Akizungumza Agosti 6, 2026, wakati wa zoezi la kutembelea wateja, kukagua na kusoma mita za maji pamoja na kufuatilia hali ya upatikanaji wa huduma katika eneo hilo, Meneja wa Mkoa wa kihuduma DAWASA Ubungo, Mhandisi Anthony Budaga, alisema zoezi hilo ni sehemu ya mkakati wa Mamlaka wa kubaini changamoto zinazowakabili wateja na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Alieleza kuwa ukaguzi huo unalenga kubaini mita zenye matumizi sifuri au matumizi madogo yasiyoendana na hali halisi, pamoja na kutathmini upatikanaji wa huduma ya maji nyumba kwa nyumba ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wakati.

“Kimara B imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa muda mrefu kutokana na ongezeko la idadi ya wakazi, huku miundombinu iliyopo ikiwa ilisanifiwa kuhudumia idadi ndogo ya watu. DAWASA imeandaa mpango wa kulaza bomba lenye uwezo mkubwa zaidi litakaloendana na mahitaji ya sasa na kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi,” amesema Mhandisi Budaga.

Aidha, amesema mradi huo utaongeza uwezo wa usambazaji wa maji, kuimarisha mtiririko wa huduma na kuhakikisha wananchi wa Kimara B wanapata huduma ya maji kwa uhakika.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimara B, Ndugu Beruki Kikwala, ameipongeza DAWASA kwa kufika eneo hilo na kufanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba, akisema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Mamlaka katika kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.

“Leo tupo pamoja na DAWASA tukikagua mita na kuangalia hali ya upatikanaji wa maji katika kila nyumba. Lengo ni kubaini sababu zinazowafanya baadhi ya wananchi wapate maji na wengine wasipate, ili changamoto hii ipatiwe ufumbuzi wa kudumu,” amesema Kikwala.

Naye mkazi wa Kimara B, Ndugu Cesilia Masangula, amesema wananchi wa eneo hilo wamepokea kwa matumaini makubwa hatua zilizochukuliwa na DAWASA, akieleza kuwa changamoto ya maji imekuwa ikiathiri maisha ya kila siku, hususan wanawake na watoto ambao hulazimika kutumia muda mwingi kutafuta maji.

Amesema utekelezaji wa mradi wa kuboresha miundombinu ya maji pamoja na ukaguzi wa mita utasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma na kuboresha ustawi wa wananchi wa Kimara B.

spot_img

Latest articles

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM REHEMA SOMBI (MNEC) APOKELEWA NKASI, AHIMIZA VIJANA KUUNGANISHA SIASA NA UCHUMI

Na Mwandishi Wetu MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Rehema Sombi Omary (MNEC), amepokelewa kwa...

DAWASA YAPELEKA TABASAMU KUNDI MAALUM WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imehitimisha wiki ya...

TANESCO YANG’ARA TUZO ZA UMAHIRI WA MAWASILIANO KWA UMMA

📌 Yanyakua tuzo nne katika vipengele mbalimbali 📌 Yatambuliwa kwa ubora katika mawasiliano ya kimkakati,...

BRELA YAFUNGUA FURSA YA URASIMISHAJI KWA WADAU WA UCHUMI WA UBUNIFU ARUSHA

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeweka kambi ya...

More like this

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM REHEMA SOMBI (MNEC) APOKELEWA NKASI, AHIMIZA VIJANA KUUNGANISHA SIASA NA UCHUMI

Na Mwandishi Wetu MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Rehema Sombi Omary (MNEC), amepokelewa kwa...

DAWASA YAPELEKA TABASAMU KUNDI MAALUM WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imehitimisha wiki ya...

TANESCO YANG’ARA TUZO ZA UMAHIRI WA MAWASILIANO KWA UMMA

📌 Yanyakua tuzo nne katika vipengele mbalimbali 📌 Yatambuliwa kwa ubora katika mawasiliano ya kimkakati,...