UKAGUZI WA MIGODI WAIMARISHA USALAMA, UHIFADHI WA MAZINGIRA

Tume ya Madini yasisitiza uchimbaji unaozingatia sheria, afya na maendeleo endelevu

Na Mwandishi Wetu

TUME ya Madini imeendelea kuimarisha ukaguzi wa migodi nchini ili kuhakikisha shughuli zote za uchimbaji zinafanyika kwa kuzingatia sheria, usalama wa wafanyakazi, afya kazini na utunzaji wa mazingira, hatua inayolenga kujenga sekta ya madini yenye tija na endelevu.

Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Mjiolojia na Mkaguzi wa Migodi kutoka Tume ya Madini, Paschal Juma, amesema Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira chini ya Mkurugenzi wake, Mhandisi Hamisi Kamando, ina jukumu la kusimamia na kufuatilia shughuli zote za uchimbaji ili kuhakikisha zinazingatia Sheria ya Madini, kanuni, sera na miongozo mbalimbali ya sekta hiyo.

Amesema Kurugenzi hiyo hufanya ukaguzi wa usalama na afya mahali pa kazi, hufuatilia utekelezaji wa mipango ya usimamizi wa mazingira, urejeshaji wa maeneo yaliyochimbwa pamoja na mipango ya ufungaji migodi kwa kuzingatia viwango vinavyolinda mazingira na kuhakikisha rasilimali za madini zinatumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha, amesema Kurugenzi hiyo hupitia na kuidhinisha mipango ya uchimbaji, taarifa za utendaji wa migodi na usanifu wa miundombinu ya migodi, huku ikisimamia matumizi salama ya baruti kwa mujibu wa Sheria ya Baruti, Sura ya 45, na kanuni zake.

Paschal amesema Tume ya Madini inatumia Maonesho ya Nanenane kama jukwaa la kutoa elimu kwa wananchi, wachimbaji na wadau wa sekta kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya kujikinga, mbinu salama za uchimbaji, utunzaji wa mazingira pamoja na uhifadhi na matumizi salama ya baruti.

Amesisitiza kuwa elimu hiyo inalenga kuongeza uelewa wa wadau, kuimarisha uzingatiaji wa sheria na viwango vya usalama, kupunguza ajali migodini na kuendeleza sekta ya madini inayochangia ukuaji wa uchumi wa taifa kwa njia endelevu.

spot_img

Latest articles

Rais Samia atuma salamu za rambirambi vifo vya polisi na mahabusu

Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuma...

NSSF YAWEKA MKAKATI WA KUFIKISHA WANACHAMA MILIONI 6.6

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeweka mkakati wa kuongeza...

ASKARI NA MAHABUSU WADAIWA KUFARIKI AJALI YA GARI LA POLISI MLIMA SEKENKE

Na Mwandishi Wetu ASKARI na mahabusu wanadaiwa kufariki dunia baada ya gari la Polisi walilokuwa...

TANESCO YAELEZA MIKAKATI YAKE YA KUKABILIANA NA ATHARI ZINAZOWEZA KUJITOKEZA WAKATI WA MVUA ZA EL NINO

📌Yaelimisha wananchi kuchukua tahadhari katika matumizi salama ya umeme kipindi cha mvua Na Mwandishi Wetu...

More like this

Rais Samia atuma salamu za rambirambi vifo vya polisi na mahabusu

Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuma...

NSSF YAWEKA MKAKATI WA KUFIKISHA WANACHAMA MILIONI 6.6

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeweka mkakati wa kuongeza...

ASKARI NA MAHABUSU WADAIWA KUFARIKI AJALI YA GARI LA POLISI MLIMA SEKENKE

Na Mwandishi Wetu ASKARI na mahabusu wanadaiwa kufariki dunia baada ya gari la Polisi walilokuwa...