WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA TPRB NANENANE DODOMA

Na Mwandishi Wetu

Na Mwandishi Wetu

WANANCHI na wadau mbalimbali wanaendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni jijini Dodoma.

Kupitia banda la TPRB lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Ardhi Village), wananchi wanapata elimu na huduma muhimu kuhusu mipangomiji.

Baadhi ya wananchi waliotembelea banda hilo wameeleza kuridhishwa na huduma wanazopata. Baraka Chacha amesema amepata uelewa mpana kuhusu majukumu ya TPRB na namna inavyosimamia weledi katika sekta ya mipangomiji.

Naye Aisa Badi, mkazi wa Makulu jijini Dodoma, amesema maonesho hayo yamemsaidia kupata elimu muhimu kuhusu upangaji wa miji, huku Ibrahimu Oso akiishukuru TPRB kwa kusogeza huduma karibu na wananchi na kutoa maelezo kwa uwazi na urahisi kueleweka.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko, alitembelea banda la TPRB na kupata maelezo ya kina kutoka kwa wataalamu wa bodi hiyo kuhusu huduma zinazotolewa pamoja na majukumu yake katika kuhakikisha mipangomiji inazingatia weledi na misingi ya kitaalamu.

Dkt. Sagamiko alipongeza juhudi za TPRB katika kuelimisha umma kupitia Maonesho ya Nanenane.

Kwa upande wake, Meneja Ufuatiliaji (Compliance Manager) wa TPRB, TP. Mathias Mkumbo, amewataka wananchi na wadau kutumia fursa ya maonesho hayo kujipatia huduma na elimu muhimu kuhusu sekta ya mipangomiji.

TP. Mkumbo ameeleza kuwa kupitia maonesho hayo, TPRB inatoa huduma mbalimbali ikiwemo kupokea maombi ya usajili, kutoa ushauri wa kitaalamu, pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa upangaji bora wa miji na makazi katika kuleta maendeleo endelevu.

Aidha, TP. Mkumbo amesema TPRB itaendelea kutoa huduma hizo kwa kipindi chote cha maonesho kuanzia Agosti 1 hadi Agosti 9, 2026, na amewataka wananchi kufika katika banda la TPRB lililopo ndani ya Ardhi Village ili kupata huduma na ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya mipangomiji.

spot_img

Latest articles

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...

MRADI WA UMEME SIMIYU KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WANANCHI

📌 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...

More like this

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...