Polisi Rufiji wahamasisha vijana kujikita katika shughuli halali za kiuchumi

Na Mwandishi Wetu, Rufiji

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji limewahimiza vijana kujikita katika shughuli halali za kiuchumi badala ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu, likisema ajira za ujasiriamali zina mchango mkubwa katika kukuza kipato na kuimarisha usalama wa jamii.

Wito huo ulitolewa na Polisi wa Kata ya Bwawani, Tarafa ya Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji, Inspekta William Anthony Mulirije alipokutana na wajasiriamali wanaojishughulisha na uchomaji wa mkaa unaotokana na mabaki ya miti, mbao na mabanzi yaliyotumika viwandani kutengeneza bidhaa mbalimbali katika Kitongoji cha Mpalange.

Inspekta Muliriye aliwataka wajasiriamali hao kuwa mabalozi wa kuwahamasisha vijana wengine kushiriki katika shughuli halali za uzalishaji na kujiepusha na uhalifu, akisisitiza kuwa vitendo vya uhalifu havina manufaa kwa mtu binafsi wala jamii.

Sambamba na hilo, aliwakumbusha wajibu wao wa kushiriki katika malezi bora ya watoto na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, hususan katika maeneo ya kazi na ndani ya jamii.

Aidha, aliwasisitiza kuzingatia usalama na afya mahali pa kazi kwa kutumia vifaa kinga dhidi ya vumbi na mazingira hatarishi ili kujilinda pamoja na kulinda afya za familia zao.

Inspekta Muliriye pia aliwahamasisha kushiriki kikamilifu katika ulinzi shirikishi na ulinzi jirani, akisema ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama ni nyenzo muhimu ya kuzuia na kutokomeza uhalifu katika maeneo yao.

Alisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na wananchi katika kutoa elimu ya uhalifu, usalama na maendeleo ya jamii ili kujenga mazingira salama yanayowezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za kiuchumi kwa amani.

spot_img

Latest articles

Wakulima wahimizwa kujiunga na Bima ya Kilimo kujikinga na hasara

Na Mwandishi Wetu, Dodoma WAKULIMA nchini wamehimizwa kujiunga na Bima ya Kilimo ili kujikinga dhidi...

BoT yatumia maonesho ya Nanenane kuhamasisha vijana kujiunga na Chuo chake

Na Mwandishi Wetu CHUO cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT Academy) kimefungua dirisha la...

VIJANA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA ZA MADINI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Na Mwandishi Wetu VIJANA nchini wamehimizwa kutumia nguvu kazi, maarifa na ubunifu wao kuchangamkia...

TTCL yatumia Nanenane kuhamasisha matumizi ya huduma za Cloud

Na Mwandishi Wetu, Dodoma SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kupitia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi...

More like this