Msajili wa Hazina akutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa EADB

Na Mwandishi wa OTR

MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, leo, Agosti 4, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) kuhusu namna benki hiyo inaweza kuimarisha mchango wake katika kuchochea maendeleo ya Tanzania.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam, Bw. Mchechu, alikutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EADB, Bw. Benard Mono, pamoja na Meneja wa Benki hiyo nchini Tanzania, Bw. Stephen Wambura.

Mazungumzo hayo yaligusia pia nafasi ya EADB katika kuwezesha uwekezaji na kukuza shughuli za kiuchumi nchini, ambapo ilielezwa kuwa benki hiyo haitoi mikopo kwa Serikali pekee, bali pia inafadhili sekta binafsi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya uwekezaji na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

EADB inamilikiwa kwa pamoja na Serikali za nchi nne wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda, zinazomiliki kwa pamoja asilimia 92 ya hisa za benki hiyo, huku asilimia nane zikimilikiwa na taasisi za fedha na maendeleo.

Kwa Tanzania, nafasi hiyo ya umiliki inatoa fursa ya kuhakikisha EADB inaendelea kuongeza mchango wake katika kuchochea uwekezaji na shughuli za kiuchumi nchini.

Kwa kutumia nafasi yake kama mwanahisa, Tanzania inaweza kushirikiana na wanahisa wengine na uongozi wa EADB katika kuwezesha fursa zaidi za uwekezaji, kuchochea ukuaji wa biashara na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya maendeleo nchini.

spot_img

Latest articles

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...

MRADI WA UMEME SIMIYU KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WANANCHI

📌 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...

More like this