WMA YAANZA KUTOA ELIMU YA VIPIMO KATIKA MAONESHO YA NANE NANE

Na Mwandishi Wetu

Wakala wa Vipimo (WMA) umeanza kutoa elimu ya vipimo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi katika siku ya kwanza, (Agosti 1, 2026) ya Maonesho ya Wakulima Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya John Malecela, eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

Kwenye banda lake lenye kaulimbiu “Usahihi wa Vipimo vya Mbegu, Pembejeo, Mazao na Bidhaa Sokoni ni Msingi wa Tija na Utekelezaji wa Dira 2050,” Maafisa Vipimo wa WMA wanatoa elimu ya vipimo na majukumu ya Wakala kwa ujumla katika kulinda haki za wakulima, wafugaji, wavuvi na wanunuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa WMA Bi. Veronica Simba alisema lengo ni kuhakikisha kila mkulima, mfugaji na mvuvi anaelewa umuhimu wa kutumia mizani na vipimo vingine vilivyohakikiwa na WMA.

“Kama unauza mahindi, mbolea au maziwa, na kama unanunua pembejeo za mifugo au samaki, kipimo sahihi ndiyo msingi wa faida. Tunataka kila mtu atoke hapa Nane Nane akiwa na uelewa wa kutambua na kudai kipimo sahihi,” alisisitiza Bi. Veronica.

Bi. Veronica aliwataka wakulima, wafugaji, wavuvi na wananchi kwa ujumla kutembelea banda la WMA katika kipindi chote cha maonesho hayo.

“Wataalamu wetu wapo hapa kutoa elimu bure. Njoo ujifunze, uulize maswali na hata kutoa maoni yako,” aliongeza.

WMA imesema itatumia kipindi chote cha maonesho hayo kuhamasisha matumizi ya vipimo sahihi kama njia moja ya kutekeleza Kauli Mbiu ya Taifa ya NaneNane 2026 “Tambua Soko, Ongeza Tija, Kutekeleza Dira 2050” na kuhakikisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi inakuwa na ushindani na uhakika wa soko.

spot_img

Latest articles

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...

MRADI WA UMEME SIMIYU KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WANANCHI

📌 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...

More like this