BRELA yatumia Nanenane kuhamasisha urasimishaji wa biashara

Na Mwandishi Wetu

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetoa wito kwa wakulima na wananchi kwa ujumla kutumia Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima ‘Nanenane’ kupata huduma za urasimishaji wa biashara, ukisema hatua hiyo itawawezesha kushiriki kikamilifu katika uchumi rasmi na kunufaika na fursa mbalimbali za kifedha na masoko.

Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma, Afisa Usajili wa BRELA, Yusuph Regio, amesema taasisi hiyo inatoa huduma zote muhimu katika banda la Wizara ya Viwanda na Biashara kuanzia Agosti 1 hadi Agosti 8 ili kuwasogezea wananchi huduma za usajili.

Alisema miongoni mwa huduma zinazotolewa ni usajili wa majina ya biashara, usajili wa kampuni, utoaji wa leseni za biashara Kundi A, leseni za viwanda pamoja na usajili wa awali wa alama za biashara (Trademark).

“Tunawahamasisha wafanyabiashara, wakulima na wananchi wote kufika katika banda la BRELA kupata huduma hizi kwa urahisi na kurasimisha shughuli zao za kiuchumi. Kilimo cha sasa ni kilimo biashara, hivyo ni muhimu shughuli hizo zikafanyika kwa kuzingatia taratibu za kisheria,” alisema Regio.

Sambamba na utoaji wa huduma hizo, BRELA pia imewataka wananchi kutumia mfumo mpya ulioboreshwa wa usajili, ulioanzishwa kuongeza ufanisi na kupunguza muda wa kupata huduma.

Regio alisema mfumo huo umeondoa changamoto zilizokuwapo katika mfumo wa awali wa ORS kwa kuruhusu huduma nyingi kufanyika kwa njia ya mtandao bila kumlazimu mteja kufika ofisini.

Alibainisha kuwa huduma zinazoweza kufanyika mtandaoni ni pamoja na uwasilishaji wa taarifa za dhamana (charges) zinazohusisha mikopo kutoka taasisi za fedha, hatua inayorahisisha upatikanaji wa huduma kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

“Mfumo huu umeongeza pia uwazi kwa kuwawezesha wananchi kupata taarifa muhimu za kampuni, ikiwemo hali ya uwasilishaji wa taarifa za mwaka (annual returns), pamoja na kuimarisha usalama wa taarifa kwa kuhakikisha wanahisa na wakurugenzi wanapata taarifa kila mabadiliko yanapofanyika katika kampuni zao,” amesema.

Amefafanua kuwa, ili kutumia mfumo huo mpya, mwananchi anatakiwa kuwa na Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN), namba ya simu inayotumika na anuani sahihi ya barua pepe.

Mwisho

spot_img

Latest articles

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...

MRADI WA UMEME SIMIYU KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WANANCHI

📌 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...

More like this

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...