MD TWANGE AWATAKA WANASHERIA WA TANESCO KUENDELEA KUSIMAMIA MAADILI NA TAALUMA

📌 Afungua Jukwaa la Wanasheria wa TANESCO jijini Mwanza

📌 Awasisitiza kutoa ushauri wa kisheria kwa wakati na kulinda maslahi ya Shirika

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange, amewataka wanasheria wa shirika kuendelea kusimamia maadili ya taaluma, kutoa ushauri wa kisheria kwa wakati na kulinda maslahi ya shirika ili kuimarisha utendaji na kuhakikisha TANESCO inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Bw. Twange ameyasema hayo wakati akifungua Jukwaa la Wanasheria wa TANESCO lililoanza Julai 28, 2026 jijini Mwanza, likiwakutanisha wanasheria kutoka Makao Makuu, Ofisi za Kanda na Kampuni Tanzu za TANESCO kwa lengo la kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kisheria yanayohusu utendaji wa shirika.

Akizungumza katika ufunguzi wa jukwaa hilo, Bw. Twange amewapongeza wanasheria hao kwa mchango wao katika kulinda maslahi ya shirika na kuhakikisha shughuli zake zinafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya. Ushauri wa kisheria unaotolewa kwa wakati umekuwa ukisaidia TANESCO kufanya maamuzi sahihi na kuepusha migogoro ambayo ingeweza kuzuilika mapema,” amesema Bw. Twange.

Amewasisitiza kuendelea kuzingatia maadili ya taaluma, kutunza siri za kazi na kutoa ushauri wa kitaalamu unaolinda maslahi ya shirika.

“Kila mmoja wetu ana wajibu wa kulinda taasisi. Kwa upande wa wanasheria, hilo linaanza na kuzingatia maadili ya taaluma, kutunza siri za kazi na kuhakikisha kila ushauri unaotolewa unalinda maslahi ya TANESCO na kuimarisha utendaji wake,” amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa TANESCO, Wakili Sundi Mahalu, amesema idara hiyo itaendelea kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kuhakikisha shughuli za shirika zinaendelea kufanyika kwa kuzingatia misingi ya utawala bora na sheria.

“Jukwaa hili linatupa nafasi ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha uwezo wetu wa kitaaluma ili tuendelee kutoa huduma bora za kisheria zinazochangia mafanikio ya TANESCO,” amesema Wakili Mahalu.

Jukwaa la Wanasheria wa TANESCO linafanyika kwa siku tatu likiwa sehemu ya mkakati wa shirika wa kuendelea kuimarisha uwezo wa wataalamu wake wa sheria, hatua inayochangia ufanisi wa utendaji, usimamizi bora wa masuala ya kisheria na ulinzi wa maslahi ya shirika.

spot_img

Latest articles

OTR na IMF zajadili utendaji wa taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa Shirika la Fedha...

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YAPUNGUA KUTOKA 98,754 HADI 33,511

Na Tatu Mohamed MAAMBUKIZI mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka watu 98,754...

MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME DEGE KUIMARISHA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KIGAMBONI

📌Wafikia Asilimia 90 katika utekelezaji wake 📌 Kukamilika Mwisho wa Mwezi Disemba 2026 Na Mwandishi Wetu...

GBT yaikaribisha BetSasa sokoni, yaitaka kuzingatia maadili

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe ameikaribisha...

More like this

OTR na IMF zajadili utendaji wa taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa Shirika la Fedha...

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YAPUNGUA KUTOKA 98,754 HADI 33,511

Na Tatu Mohamed MAAMBUKIZI mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka watu 98,754...

MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME DEGE KUIMARISHA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KIGAMBONI

📌Wafikia Asilimia 90 katika utekelezaji wake 📌 Kukamilika Mwisho wa Mwezi Disemba 2026 Na Mwandishi Wetu...