TPDC kuongeza uzalishaji wa gesi kupitia visima vipya

Na Mwandishi Wetu

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema linatarajia kuongeza uzalishaji wa gesi asilia nchini kupitia mradi wa uchorongaji wa visima vitatu katika Kitalu cha Mnazi Bay, ambapo visima viwili tayari vimekamilika na kimoja kinaendelea kuchorongwa.

Akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Mjiolojia wa TPDC, Magambo Samweli, alisema visima hivyo vinachimbwa kwa ubia kati ya TPDC na kampuni ya Maurel & Prom (M&P) kwa lengo la kuongeza kiwango cha gesi kinachozalishwa katika kitalu hicho.

Alisema kati ya visima vitatu vinavyochimbwa, viwili vinalenga kuongeza uzalishaji wa gesi, huku kisima kimoja kikitumika kutafuta maeneo mapya yenye akiba ya gesi asilia.


Kwa mujibu wa Samweli, kisima kimoja kina uwezo wa kuzalisha futi za ujazo milioni 40 za gesi kwa siku, huku kingine kikitarajiwa kuzalisha futi za ujazo milioni 60 kwa siku, hatua itakayoongeza upatikanaji wa gesi kwa matumizi mbalimbali nchini.

Mbali na mradi wa Mnazi Bay, TPDC kwa kushirikiana na kampuni ya ARA Petroleum inaendelea kuendeleza Kitalu cha Ruvuma, ambako tayari kumekuwa na ugunduzi mkubwa wa gesi katika eneo la Ntorya.

Alisema kwa sasa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka visimani hadi Kituo cha Kuchakata Gesi cha Madimba unaendelea.

“Bomba hilo lenye urefu wa kilomita 34.2 na kipenyo cha inchi 14 litasafirisha gesi kutoka vitalu vya Ntorya na Ruvuma kwenda Madimba kwa ajili ya kusafishwa kabla ya kuingizwa kwenye bomba kuu la taifa linalopeleka gesi hadi Dar es Salaam,” alisema.

Samweli alisema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kukamilika kati ya Novemba na Desemba mwaka huu, huku usafirishaji wa gesi kupitia bomba hilo ukitarajiwa kuanza mwezi Desemba 2026.

Alieleza kuwa kuanza kwa uzalishaji kutoka kwenye visima vipya kutaongeza kiwango cha gesi kinachoingia kwenye bomba kuu la taifa, hatua itakayosaidia kuongeza upatikanaji wa gesi kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwandani, magari yanayotumia gesi pamoja na matumizi ya majumbani.

Alisema TPDC itaendelea kushirikiana na wawekezaji katika kuharakisha utafutaji na maendeleo ya rasilimali za gesi asilia ili kuhakikisha nchi inanufaika zaidi na nishati hiyo katika kukuza uchumi na maendeleo ya viwanda.

spot_img

Latest articles

STAMICO YAONGEZA MAPATO HADI SH BILIONI 147.8

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeongeza mapato yake ya ndani kutoka...

SERIKALI KUANZA UTAFITI WA MADINI ENEO KUBWA LA NCHI KWA KUTUMIA FEDHA ZA NDANI

Ni kupitia mfuko wa utafiti wa Madini ▪️Rais Samia apongezwa kwa dhamira ya kukuza sekta...

NDEJEMBI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA UMEME IGANJO, MBEYA

📌 Ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 93 ya utekelezaji 📌 Aeleza manufaa ya mradi...

WAZIRI MKUU ASISITIZA AFRIKA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA USAFIRI WA MAJINI

Na Tatu Mohamed WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema nchi za Afrika zinapaswa kuimarisha ushirikiano...

More like this

STAMICO YAONGEZA MAPATO HADI SH BILIONI 147.8

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeongeza mapato yake ya ndani kutoka...

SERIKALI KUANZA UTAFITI WA MADINI ENEO KUBWA LA NCHI KWA KUTUMIA FEDHA ZA NDANI

Ni kupitia mfuko wa utafiti wa Madini ▪️Rais Samia apongezwa kwa dhamira ya kukuza sekta...

NDEJEMBI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA KITUO CHA UMEME IGANJO, MBEYA

📌 Ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 93 ya utekelezaji 📌 Aeleza manufaa ya mradi...