DIB yawaita wananchi kupata elimu ya amana

Na Mwandishi Wetu

BODI ya Bima ya Amana (DIB) imewahimiza wananchi kutembelea banda lake katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) ili kujifunza kuhusu haki zao na namna amana zao zinavyolindwa pindi benki au taasisi ya fedha inapofungwa.

Wito huo umetolewa na Afisa wa Bodi ya Bima ya Amana, Joyce Shala, ambapo amesema DIB inatatumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu ya bodi hiyo na umuhimu wa bima ya amana katika kuimarisha imani ya wananchi kwa sekta ya fedha.

“Niwasihi wananchi kutembelea banda la Bodi ya Bima ya Amana ili kupata elimu kuhusu haki zao na namna amana zao zinavyolindwa. Mfumo huu unaongeza imani katika sekta ya benki na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa,” amesema.

Amefafanua kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kutumia huduma za benki na taasisi za fedha bila hofu, kwa kuwa amana zao zinalindwa na Bodi ya Bima ya Amana endapo taasisi ya fedha itafungwa na kuwekwa chini ya ufilisi na Benki Kuu ya Tanzania.

Aidha, amesema bodi hiyo hukusanya michango kutoka kwa benki na taasisi za fedha ili kuimarisha Mfuko wa Bima ya Amana, ambao hutumika kulipa fidia kwa wateja pale benki inapofungwa na kuwekwa chini ya ufilisi.

“Mbali na kulipa fidia, Bodi ya Bima ya Amana pia husimamia ufilisi wa benki zilizofungwa kwa kukusanya mali zake na kulipa wadai kwa mujibu wa sheria, wakiwemo wateja wenye amana zinazozidi kiwango kinacholindwa na bima,” amesema.

Amebainisha kuwa tangu mwaka 2015 bodi hiyo iliongezewa jukumu la kupunguza hasara katika utatuzi wa migogoro ya benki na taasisi za fedha zinazokabiliwa na changamoto za kiuendeshaji, hatua inayolenga kuimarisha uthabiti wa mfumo wa fedha nchini.

Bodi ya Bima ya Amana ilianza shughuli zake rasmi mwaka 1994 chini ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha, ikiwa na jukumu la kulinda amana za wateja wa benki na taasisi za fedha zilizopewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

spot_img

Latest articles

Waziri Katambi anatengeneza janga kubwa

MEI mwaka huu picha mjongeo ya mahojiano kati ya Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu,...

Waziri Mkuu: Kafulila kiongozi kijana mwenye upeo mpana

Amtaja Kama Kiongozi Kijana Mwenye Exposure ya Kimataifa Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu wa Jamhuri...

VETA Kihonda yaja na mashine ya kisasa ya kulimia

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Ufundi stadi (VETA) Kihonda, imebuni mashine...

WATANZANIA KUNUFAIKA NA UMEME WA UHAKIKA; MRADI WA CHALINZE–DODOMA WAFIKIA ASILIMIA 89 YA UTEKELEZAJI

📌 utaimarisha upatikanaji wa umeme kwa wananchi, viwanda na shughuli za kiuchumi 📌 Wananchi wanatarajiwa...

More like this

Waziri Katambi anatengeneza janga kubwa

MEI mwaka huu picha mjongeo ya mahojiano kati ya Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu,...

Waziri Mkuu: Kafulila kiongozi kijana mwenye upeo mpana

Amtaja Kama Kiongozi Kijana Mwenye Exposure ya Kimataifa Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu wa Jamhuri...

VETA Kihonda yaja na mashine ya kisasa ya kulimia

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Ufundi stadi (VETA) Kihonda, imebuni mashine...