VETA Kihonda yaja na mashine ya kisasa ya kulimia

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Ufundi stadi (VETA) Kihonda, imebuni mashine ya kisasa ya kulimia maarufu kama Pawatira, ili kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kupunguza changamoto zinazowakabili shambani.

Akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba), Mkufunzi Mwandamizi wa VETA Kihonda, Fredrick Uliki, amesema mashine hiyo ilibuniwa baada ya utafiti wa kina kubaini kuwa baadhi ya mashine zinazoagizwa kutoka nje hazikidhi kikamilifu mazingira ya kilimo nchini Tanzania.

“Tulifanya utafiti na kubaini kuwa mashine nyingi zinazoagizwa kutoka nje hazina uimara wa kutosha kufanya kazi kwa muda mrefu katika mashamba ya mabondeni na maeneo yenye milima. Kutokana na changamoto hiyo, tukabuni teknolojia inayokidhi mazingira yetu na mahitaji ya wakulima wa Tanzania,” amesema Uliki.

Ameeleza kuwa Pawatira imeundwa mahsusi kwa ajili ya kurahisisha kilimo cha mboga mboga, hasa katika maeneo ya mabondeni ambako matrekta makubwa hushindwa kufika kutokana na hali ya ardhi.

“Tofauti na matrekta makubwa, mashine hii inaweza kufanya kazi kwa urahisi katika maeneo hayo na kuwasaidia wakulima kuongeza tija na kupunguza gharama za uzalishaji,” ameongeza.

Mbali na kilimo cha mboga mboga, Uliki amesema mashine hiyo pia inafaa kwa kilimo cha mpunga kwa kuwa ina uwezo wa kugandua ardhi na kulainisha udongo kwa ufanisi, hali inayowezesha mbegu kuota haraka na kuongeza mavuno.

“Mashine hii ina uwezo wa kulima hadi hekta tatu kwa siku, kutegemeana na nguvu ya mtumiaji, aina ya udongo na jiografia ya eneo husika. Maeneo yenye tambarare huruhusu kazi kufanyika kwa kasi zaidi kuliko maeneo yenye miteremko au mabondeni,” amesema.

Akizungumzia matengenezo, Uliki amesema wakulima hawatakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa vipuri kwa kuwa spea za mashine hiyo zinapatikana kwa urahisi katika mikoa mbalimbali nchini kwa bei nafuu.

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha ubunifu huo unakuwa suluhisho la kudumu katika kuongeza ufanisi wa shughuli za kilimo na kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.

spot_img

Latest articles

DIB yawaita wananchi kupata elimu ya amana

Na Mwandishi Wetu BODI ya Bima ya Amana (DIB) imewahimiza wananchi kutembelea banda lake katika...

Waziri Mkuu: Kafulila kiongozi kijana mwenye upeo mpana

Amtaja Kama Kiongozi Kijana Mwenye Exposure ya Kimataifa Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu wa Jamhuri...

WATANZANIA KUNUFAIKA NA UMEME WA UHAKIKA; MRADI WA CHALINZE–DODOMA WAFIKIA ASILIMIA 89 YA UTEKELEZAJI

📌 utaimarisha upatikanaji wa umeme kwa wananchi, viwanda na shughuli za kiuchumi 📌 Wananchi wanatarajiwa...

Gawio la serikali laongezeka kwa asilimia 30

Na Mwandishi wa OTR Dar es Salaam. Gawio na michango mingine ambayo Serikali imepokea kutoka...

More like this