UKARABATI WA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA HALE WAFIKIA ASILIMIA 83 YA UTEKELEZAJI

📌 Waziri Ndejembi amtaka mkandarasi kukamilisha ukarabati kwa wakati bila kuongezewa muda wa mkataba

📌 Kukamilika kwake kutaongeza ufanisi wa uzalishaji na kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika Mkoa wa Tanga na maeneo ya jirani

Na Mwandishi Wetu, Korogwe – Tanga

Serikali imeendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa miundombinu ya umeme nchini, huku Mradi wa Ukarabati wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Hale wilayani Korogwe, mkoani Tanga, ukifikia asilimia 83 ya utekelezaji.

Akikagua maendeleo ya Mradi huo tarehe 29 Juni, 2026 Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb), amemtaka mkandarasi kuhakikisha anakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa, akisisitiza kuwa Serikali haitakuwa tayari kuongeza muda wa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo.

Waziri Ndejembi amesema kukamilika kwa ukarabati wa Kituo cha Hale kutaimarisha ufanisi wa uzalishaji wa umeme, kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuchochea shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Tanga na maeneo ya jirani.

“Mkandarasi ahakikishe anakamilisha mradi huu kwa muda uliopangwa ifikapo Julai 31 mwaka huu, ili wananchi waanze kunufaika na huduma ya umeme wa uhakika pamoja na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi,” amesema Mhe. Ndejembi.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji Umeme TANESCO, Mhandisi Timoth Mgaya, amesema mradi huo unagharimu dola za Kimarekani milioni 24.81, sawa na takribani shilingi bilioni 64, na hadi sasa umefikia asilimia 83 ya utekelezaji.

“Mradi huu unagharimu dola milioni 24.81 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 64. Hadi sasa utekelezaji umefikia asilimia 83, na tunaendelea kushirikiana na mkandarasi kuhakikisha kazi zilizobaki zinakamilika ndani ya muda uliopangwa,” amesisitiza Mhandisi Mgaya.

Mradi wa ukarabati wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Hale unalenga kuongeza ufanisi wa kituo hicho, kuboresha utegemevu wa uzalishaji wa umeme na kuendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme wa uhakika kwa wananchi.

Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Hale ni kituo cha kwanza cha kuzalisha umeme kwa kutumia maji nchini. Kilijengwa kati ya mwaka 1961 na 1964 na kina uwezo wa kuzalisha takribani megawati 21. Ukarabati unaoendelea unalenga kuongeza ufanisi wa kituo hicho ili kiendelee kutoa mchango mkubwa katika Gridi ya Taifa kwa miaka ijayo.

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...