Makonda  awajibu wanaoponda ziara ya Rio

Na Winfrida Mtoi

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema ziara ya beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand nchini si kwa ajili ya ‘kuposti’ katika mitandao yake ya kijamii, bali kuona vipaji vya kitanzania kupitia taasisi yake na kusaidia kuvipaisha duniani.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Mei 22, 2026 baada ya kuwepo kwa mijadala juu ya mchezaji huyo kutoposti ziara yake ya Tanzania katika mitandao yake ya kijamii.

Waziri huyo ameweka bayana kuwa ndiye alimuomba Rio asiposti chochote, kwani ndoto yake ilikuwa ni kumleta kusaidia vijana katika kuendeleza vipaji vyao kimataifa kwa sababu mchezaji huyo anajua kona zote za dunia.

“Agenda kubwa inayoendelea mjini hasa nchini ni Rio kuposti, kwa nini Rio hajaposti ni posti gani unataka Rio aposti pale? Tunapenda kujadili mambo kwa kuyaona bila kuyajua, tunaamini tunajua kila kitu.

“Ushawahi kufikiri mtu uko naye, anaongelea mema juu ya nchi yako, anaongelea juu ya serikali inayopiga hatua alafu wewe badala kuchukua ile posti uipeleke duniani unataka aposti yeye. Akiposti yeye ndio utajua yuko Tanzania?,”

Amesisitiza kuwa posti ni siku moja lakini akimtoa mtoto mmoja wa kitanzania ni mafanikio makubwa, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana na watu wakubwa duniani kuitangaza Tanzania.

spot_img

Latest articles

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...

MRADI WA UMEME SIMIYU KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WANANCHI

📌 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...

More like this