Tanesco yaendelea kuwaelimisha wanaofanya shughuli za kiuchumi kwenye miundombinu ya umeme

📌Ni katika muendelezo wa ukaguzi wa miundombinu ya umeme Dar es salaam

📌Yatoa rai kwa wananchi kuondoka kwa ajili ya usalama wa maisha na mali zao

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kuwasisitiza wananchi wanaofanya shughuli zao za kiuchumi katika miundombinu ya umeme kuondoka katika maeneo hayo kwa hiari, kwa kuwa wanahatarisha usalama wa maisha na mali zao.

Akizungumza katika muendelezo wa zoezi la kukagua miundombinu ya umeme Mei 18, katika eneo la Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, Msimamizi Msaidizi wa Njia Kuu za Kusafirisha Umeme Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Nicholaus Kivelege, amesema TANESCO inafanya jitihada za makusudi kutoa elimu kuhusu athari za kuendelea kufanya shughuli za kiuchumi chini ya njia kubwa za kusafirisha umeme katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema licha ya jitihada hizo, bado baadhi ya wananchi wanaendelea kufanya shughuli hizo, hivyo amewaomba viongozi wa serikali za mitaa katika maeneo husika kuongeza nguvu ya kutoa elimu kuhusu madhara yanayoweza kujitokeza kwa wananchi wanapofanya shughuli zao katika miundombinu ya umeme.

“TANESCO tunaendelea na zoezi la ukaguzi wa miundombinu ya umeme katika maeneo ya Mbagala Zakhem, tunafanya jitihada kubwa kutoa elimu, lakini bado kuna ugumu kwa baadhi ya wananchi. Tunaomba viongozi wa serikali za mitaa watusaidie katika zoezi hili ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza,” alifafanua Bw. Kivelege.

Baadhi ya wananchi, akiwemo Bw. Zahali Maulidi wa maeneo ya Mbagala, licha ya kufahamu kuwa kufanya shughuli chini ya miundombinu ya umeme ni hatari, wameiomba Serikali kuangalia namna ya kuwatafutia maeneo mengine ya kufanyia kazi zao ili waweze kuondoka katika maeneo hatarishi.

“Kwanza niwapongeze TANESCO kwa kuendelea kutoa elimu. Sisi tuko tayari kuhama maeneo haya endapo tutatafutiwa eneo jingine. Tunafahamu kuwa ni hatari kufanya shughuli za kiuchumi katika miundombinu ya umeme,” alifafanua Bw. Maulidi.

Haya yamejiri wakati TANESCO ikiendelea na mkakati wa kutoa elimu kuhusu athari za kufanya shughuli za kiuchumi katika miundombinu ya umeme, ili wananchi waweze kuondoka wenyewe kwa hiari kwa ajili ya usalama wa maisha yao.

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...