Mradi wa njia ya kusafirisha umeme Chalinze-Dodoma kukamilika Agosti 2026: MD Twange

Utekelezaji wa Mradi wafikia asilimia 82.5

📌Shilingi bilioni 514 kutumika ajili utekelezaji wa mradi

📌 Amtaka Mkandarasi kuongeza kasi mradi huo wa kimkakati ukamilike kwa wakati

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, amesema mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Zuzu, Dodoma, unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 18, 2026.

Akizungumza Mei 20, 2026 wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo katika mikoa ya Morogoro na Dodoma, Bw. Twange amesema mradi huo ni muhimu kwa kuwa unasafirisha umeme unaozalishwa moja kwa moja kutoka katika Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere ambao unapita Chalinze hadi Dodoma.

Amesema utekelezaji wa mradi huo unaenda sambamba na upanuzi wa vituo vya kupokea na kupoza umeme vya Chalinze na Zuzu, Dodoma, ambapo kukamilika kwake kutaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme kwa ajili ya shughuli za uwekezaji pamoja na kuongeza fursa mbalimbali za kiuchumi nchini.

Amesema Serikali Chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Shilingi Bil 514 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huo ambao utachochea shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kuendana na kasi ya ongezeko la mahitaji.

“Leo tumefanya ukaguzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma. Njia hii ni muhimu kwa kuwa inaongeza uwezo wa kusafirisha umeme kutoka Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere kwenda kwa watumiaji mbalimbali. Idadi ya watu imeongezeka na shughuli za kiuchumi zimeongezeka hivyo tumeingia makubaliano sasa mradi huu utakamilika Agosti 18, 2026,” alisisitiza Bw. Twange.

Ameeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa huku akimtaka mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.“Tumekubaliana kuongeza wataalamu na vifaa vya kutosha ili kuhakikisha mradi huu unakamilika ndani ya muda ulioainishwa ,” ameongeza.

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi, Mhandisi Newtone Lingstone, amesema mradi huo wenye urefu wa kilometa 345 Kutoka Chalinze hadi Dodoma unafadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania, huku kazi za upanuzi wa vituo vya kupokea na kupoza umeme vya Chalinze na Dodoma zikiendelea vizuri.

Kukamilika kwa mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma wenye msongo wa Kilovoti 400 utaimarisha na hali ya upatikanaji wa umeme si kwa Mkoa wa Dodoma pekee, bali katika maeneo mbalimbali nchini.

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...