DAWASA yaja na operesheni siku 90 kudhibiti upotevu wa maji

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetenga siku 90 za kutekeleza mpango maalum wa kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha huduma ya majisafi na kuongeza ufanisi wa miundombinu yake.

Akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa kudhibiti upotevu wa maji, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, amesema Mamlaka imejiwekea siku 90 za kupambana na upotevu wa Maji na hatua za awali zimeanza kwa ukarabati na ubadilishaji wa miundombinu chakavu inayochangia mivujo na upotevu mkubwa wa maji katika maeneo mbalimbali ya kihuduma.

“Kama mnavyofahamu, Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) alitoa taarifa kuwa kiwango cha upotevu wa maji katika Mamlaka nyingi nchini kimefikia asilimia 35. Kutokana na hali hiyo, DAWASA tumeanza kuchukua hatua mahsusi kwa kutenga siku 90 za kushughulikia changamoto hii,” amesema Mhandisi Bwire.

Ameeleza kuwa mafanikio ya mpango huo yatategemea ushirikiano wa karibu kati ya DAWASA na wananchi, huku Mamlaka ikiahidi kutoa zawadi kwa watu watakaosaidia kutoa taarifa za mivujo ya maji na maeneo yenye upotevu mkubwa wa huduma hiyo.

“Katika utekelezaji wa mpango huu tutashirikisha wadau mbalimbali, wakiwemo watumiaji na wasiokuwa watumiaji wa huduma ya maji, pamoja na makundi maalum kama mama lishe, maafisa usafirishaji (Bodaboda), viongozi wa serikali na jamii kwa ujumla,” ameongeza.

DAWASA imebainisha kuwa lengo lake ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 kiwango cha upotevu wa maji kinashuka hadi kufikia asilimia 20, kiwango kinachokubalika kimataifa katika sekta ya maji.

Mpango huo unatajwa kuwa sehemu ya mikakati ya muda mrefu ya Mamlaka katika kuboresha usimamizi wa maji, kuongeza mapato, kulinda rasilimali ya maji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya uhakika kwa ufanisi zaidi.

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...