Jumba la maajabu laiponza Yanga,  yapigwa faini  milioni 30,  Meneja  matatani

Na Mwandishi Wetu

KLABU ya Yanga imetozwa faini ya Sh 30 milioni  kwa kosa la wachezaji  na maofisa wa benchi la ufundi kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo,  badala yake kutumia nyumba iliyopo nje ya uwanja huo upande wa pili wa barabara.

Tukio hilo lilitokea Mei 3, 2026 wakati wa mchezo wa Derby  ya Kariakoo dhidi ya Simba uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Kwa mujibu taarifa ya  Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Tanzania iliyotolewa leo Mei 11, 2026 na  Bodi ya Ligi  (TPLB), kitendo hicho ni ukiukwaji wa Kanuni za Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Mbali na adhabu hiyo, Yanga pia imepewa onyo kali baada ya kuchelewa kuwasili uwanjani kwa mchezo huo, ikifika saa 10:35 alasiri badala ya saa 10:30 alasiri kama kanuni zinavyotaka.

Katika hatua nyingine, Meneja wa Yanga, Walter Harson, amefungiwa michezo mitatu pamoja na kutozwa faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kumsukuma mchezaji wa Simba, Clatous Chama, wakati wa mchezo huo.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this