Waziri Mkuu ahimiza ufungaji kamera  viwanjani kudhibiti ushirikina

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu, Dk.Mwigulu Nchemba, amehimiza ufungaji wa kamera nyingi katika viwanja vya michezo, ikiwamo uwanja Arusha ili kudhibiti vitendo vya ushirikina na imani potofu.

Amesema hayo leo Aprili 17, 2026, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya katika uwanja wa Arusha utakaotumika kwa michuano ya AFCON 2027.

Amesema ni muhimu kuhakikisha kila eneo la uwanja linaonekana wazi, akieleza kuwa hata vitendo vidogo visivyofaa vinapaswa kubainika mapema kupitia mifumo ya ufuatiliaji.


“Uwanja uwe na kamera nyingi, hata mtu akiweka sindano aonekane ili tukomeshe ushirikina wa ndani ya viwanja, nuru iwe ndani na nje uwanja,” amesema.  Pia Waziri Mkuu ametoa maagizo ya uharakishwaji wa mradi huo pamoja na matumizi stahiki ya fedha za ujenzi wa uwanja huo ili ukamilike, kuendana na muda wa maandalizi waliopewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

“Kaguzi zitakuja mapema zaidi ya hapa. Fanyeni kazi usiku na mchana. Tusiweke dosari ambazo hazihusiani na maandalizi ya viwanja. Ongezeni vitendea kazi, ongezeni nguvu kazi ili tutekeleze mapema huo muda ambao tumeuweka.

“La pili tuendelee kuzingatia thamani na viwango vya fedha. Tutimize mahitaji na matakwa ya waendesha shughuli wa AFCON lakini lazima tuwape thamani ya viwango Watanzania ambao ndio watoa fedha ya ujenzi,” amesema Mwigulu.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...