Na Mwandishi Wetu
DROO ya hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho, imefanyika leo Aprili 17, 2026, jijini Dar es Salaam, ambapo Simba imepangwa dhidi ya TRA United huku Yanga ikipewa JKT Tanzania.
Kwa upande wa Azam FC watakuwa wageni, Mashujaa FC katika dimba la Lake Tanganyika, wakati Singida Black Stars itakutana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Akizungumzia ratiba hiyo, Ofisa Habari wa JKT Tanzania, Masau Bwire ametamba kuwa hawaihofii kupangwa na Yanga na wamefurahia, anaamini malengo yao yatatimia ya kufika fainali baada ya msimu uliopita kuishia nusu fainali.
“Mechi yetu ya mwisho na Yanga pale KMC yaliwashitua wengi, kuwaonesha ya kwamba sisi tuko vizuri kuliko Yanga, tunakwenda kuwaonesha Watanzania, hadi hapa mechi na Yanga tushamaliza. Nina hakika kichapo cha kizalendo kitaonekana,” amesema. Masau.


